Ruto Awaonya Polisi Kuhusu Mauaji ya Raia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Rais wa Kenya, William Ruto amewaonya maafisa wa polisi dhidi ya mauaji ya kiholela ya waandamanaji wanaoipinga serikali, huku upande mwingine akisisitiza kwamba kila mtu lazima afuate sheria zilizowekwa.

Akizungumza katika ziara yake katika Kaunti ya Murang'a, Ruto ameshikilia msimamo wa serikali yake kukabiliana na wavunja sheria iwe katika vyombo vya usalama au hadharani kuhusiana na maandamano yanayoendelea yakiongozwa na upinzani.

Amerejea ahadi yake ya kutokomeza utovu wa nidhamu na kuhakikisha utawala wa sheria unazingatiwa na kuongeza kuwa ataleta utulivu nchini humo na hakuna mtu atakayeruhusiwa kusababisha ghasia, fujo na uharibifu wa mali.

“Tunaomba maafisa wetu wa kusimamia sheria wawe waangalifu, wasimame na ninataka kupongeza vyombo vyetu vya usalama kwa kuwa na weledi wa jinsi ambavyo vimewashughulikia watu hawa. Wahalifu lazima washughulikiwe kwa uthabiti na kuhakikisha kwamba kila mtu anaheshimu utawala wa sheria.”

Zaidi tembelea swahilitimes.co.tz
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad