Kocha Gamondi Kiboko Unaambiwa Bado Hajaridhika na Washambuliaji Yanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kocha Gamondi Kiboko Unaambiwa Bado Hajaridhika na Washambuliaji Yanga


Yanga imeanza msimu mpya kwa kasi ikigawa dozi kwenye michuano mbalimbali inayoshiriki, lakini kama unadhani kocha Miguel Gamondi ameridhika na kasi hiyo unakosea, kwani ametoa agizo akitaka aletewe straika mmoja amalize kazi.

Ipo hivi. Licha ya Yanga kumsajili Hafiz Konkoni bado kiwango chake hakijakata kiu ya kocha wake huku akiwa ameshafunga mabao mawili kwenye kikosi hicho.

Chanzo makini ndani ya Yanga kimesema bado tu wanaendelea kutafuta mshambuliaji taratibu, ni kweli timu inashinda kwa mabao ya kutosha lakini kocha (Gamondi) anataka ufanisi zaidi wa kutumia nafasi ambazo wanatengeneza.

Kocha (Gamondi) anataka mshambuliaji ambaye kwenye nafasi tatu atafunga mbili au zote anaona timu inatengeneza nafasi zaidi ya ushindi ambao tunaupata. Hata hivyo, kwa sasa Yanga imefungiwa kusajili kutokana na kushindwa kumlipa stahiki yake, kiungo Gael Bigirimana.

Mbali na kesi hiyo, pia Yanga inakabiliwa na mtihani mwingine baada ya beki, Mamadou Doumbia aliyevunjiwa mkataba naye kukimbilia Fifa kushtaki.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad