Zamaradi Ajibu Kuhusu Shutuma za Mange Kimambi za Kumdhulumu Mfanyakazi wake Milioni 19 za Mshahara

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Zamaradi Ajibu Kuhusu Shutuma za Mange Kimambi za Kumdhulumu Mfanyakazi wake Milioni 19 za Mshahara

Ameandika Haya Zamaradi Mketema:

Sikuwa na sababu ya kujibu hili lakini kwasababu limehusisha Brand yangu nitaliaddress kama lilivyoletwa kwa heshima ya TINAOFANYA KAZI PAMOJA

KWANZA HAKUNA MTU ANAEWEZA KUFANYA KAZI KWA MTU MIEZI 24 (miaka miwili) bila kulipwa na akaendelea kufanya kwa moyo, kama ni mimi tu alinitegemea ALIISHIJE!!? ALISURVIVE VIPI!?? Kiufupi ukweli uko hivi, HUYO HAKUWA MUAJIRIWA WANGU ILA NI MFANYAKAZI HURU na ndiomana alikaa kwa amani zote, ukipita kwenye page yake utathibitisha hilo maana ana clip za CLOUDS, za Cocacola, za kitambaa cheupe na nyingi nyingine, Harusi za watu nk, ikiwa ni mimi tu nimemuajiri iweje nikubaliane na hilo!? Yeye kutoka kufanya kazi za wengine bila kusemwa, kiufupi yeye alikuwa DAY WORKER na kijiwe chake kilikuwa ZAMARADI TV!!! Lakini pia kwanini akubaliane na kutolipwa na bado akadeliver!! Ukweli hauko hivyo, alikuwa anapewa kwa jinsi anavyofanya kazi na sio kinyume na matakwa yake ndivyo tuliishi, JIULIZE mwezi wa kwanza unapita, wa pili unapita, wa 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9 mwaka unaingia mara mwaka mwingine wa pili mtu yupo tu!!!! Halipwi haliyakuwa ni muajiriwa na haondoki!!? Inamana HATA SUMNI kweli, na anakuja kwa raha zote ninapomuhitaji, Kwanini asilalamike kipindi hiko!? kwanini alalamike atunge madai baada ya kufukuzwa!!! MILIONI 19 anayodai ni ya nini!?? Na mbona hakuwahi hata kuigusia kabla ndio kwanza naisikia baada ya kumsimamisha!!? Kiufupi he never saw this coming sababu NILIMTHAMINI SANA mpaka akafeel ENTITLED na akaniweka kwenye position ya SIWEZI BILA YEYE kwakuwa kila kitu muhimu na cha kuonekana nilikiaddress kwake (na ndivyo alivyokuwa anataka) pamoja na utendaji kazi kitabia hakuwa mzuri lakini nilimvumilia na kuishi nae kwa upendo mpaka NILIPOSHINDWA!! Hivyo Hii ni reaction baada ya mimi kumsimamisha kazi na kutokujihusisha nae kabisa ambayo hakutegemea sababu alijiamini sana, na zaidi ameshtuka baada ya kuona kile kifaa cha ofisi (LAPTOP) nahitaji kukichukua ambacho huwa kinamsaidia kwenye kazi nyingine, imekuwa ghafla ananidai MILIONI 19!!!! 😧


KUHUSU MKATABA - 

Mkataba PEKEE niliowahi kuingia nae ni 2020 mpaka 2021 nilivyokuwa Online ambayo haukuwahi kupita mwezi hajalipwa (nashukuru amekiri) baada ya mkataba kuisha nilimuacha Huru sababu nilisimamisha ofisi kwa muda hivyo sikutaka kumfunga mtu na aliendelea na shughuli zake nyingine zisizonihusu kama kawaida, nilichokuwa nafanya ni kumuita tu nilipomuhitaji na kumalizana nae kwa siku husika (tena zaidi kazi za kibalozi) maana sikuwa na kazi nyingi ikitokea kwa mwezi labda mara moja, (interview nilisimamisha sababu nilikuwa naelekea mainstream hivyo nikafocus na investment ya huku) baada ya kutoka Online na kwenda Mainstream ndipo aliporudi, na bado mimi na yeye ndani ya miezi mitatu ya mwanzo hatukuwa na mkataba bado (tulielekea huko) lakini ndani ya kipindi hiko nimeshasolve shida zake nyingi sana, kinachotokea akiwa na shida ananiambia na ninamtimizia kama ubinaadamu unavyotaka, na ninapokuwa nimebanwa namwambia sitaweza (maana nadeal na watu sio chini ya 30 na wote nasolve mambo yao kwa nyakati tofauti) hiyo anayoulizia kwenye message ni msaada wa KODI YA NYUMBA ambao aliomba na nikampatia na ndio message ya kushukuru ameituma ambayo nasikitika kwako hajaionesha 😊’


Kuhusu Kumblock SIJAMBLOCK sababu ya kudaiwa, nimemblock sababu NILIMSIMAMISHA kutokana na utovu wa nidhamu mara kadhaa na kukosa ushirikiano na wengine na kulalamikiwa kwa tabia nyingi zisizopendeza, nilimuonya zaidi ya mara tatu tena kwa kikao na mwingine mara nyingine, na mwisho ni JUMANNE NILIMSIMAMISHA RASMI KUFIKA OFISINI, na baada ya kumsimamisha niliamuru atolewe kwenye magroup yote ya ofisi, na nikaamuru LAPTOP YA OFISI aliyokuwa nayo yeye kikazi irudishwe ofisini sababu si miongoni mwetu kitu kilichomshtua maana ndio inayomsaidia hata kwenye kazi zake za nje (Alikuwa ni mfanyakazi hurui) na zaidi message alizokurupuka nazo za madai (ambayo siyafahamu) amezituma ALHAMISI NA IJUMAA kupitia I message, wakati kabla ya hapo aliahidi Kurudisha laptop kupitia Mume wangu aliempigia, lakini ghafla akabadilika na kutuma hizo message Ijumaa, na mimi nimemblock JUMANNE kabla ya hizo message hivyo kusema nimemblock kwasababu ya kudaiwa ni UONGO, nilimblock sababu sikutaka kujihusisha nae kwa chochote baada ya mengi pamoja na kuishi nae kama DADA NA MDOGO MTU!!!

Hapa katikati nilienda nae DUBAI kwa ajili ya kufata vifaa vya production, Kabla sijasafiri nae kufata Vifaa kwa siku tulikuwa tunatumia sio chini ya LAKI NANE kama tuna production kubwa!! Kuanzia mwezi wa tano tulipozindua mpaka JUZI nilipokamilisha vifaa, tulichokuwa tunafanya ni KUKODI BAADHI YA VIFAA na kuwalipa kwa wiki au mwezi!! Ni kawaida kwa maofisi kulipa baada, Nilichoshangaa ni yeye kuchukua baadhi ya message za kunikumbushia watu wa vifaa na kukata nusu kisha kupotray kama jambo analonidai kitu ambacho HAKIJAWAHI KUWEPO.. kama ana message inaonesha ZAMA kwasasa imefika hata milioni mbili deni angeonesha, lakini hamna, anavhofanya anachukua za production, yeye ndio nilimpa jukumu la kufatilia na ndio alikuwa akiniletea Bill zetu, sasa kakata message za BILL ameziweka kama vile ndizo alizokuwa ananidai (nilijua ni nyoka lakini sikuwahi kujua katika namna hii)

YES nimemfungulia kesi sababu nahitaji Laptop ya ofisi ambayo haikuwa na maana yeye kukaa nayo tena sababu hafanyi kazi zangu, na mara ya kwanza alikubali atairudisha lakini ghafla kabadilika Alhamisi na Ijumaa, KAMA ALIKUWA ANANIDAI KWANINI JUMANNE HIYO ASITUME MESSAGE KUSEMA NIPE PESA YANGU ILA ALIKUBALI ATAIRUDISHA!!? Badala yake kakaa siku mbili mbele katunga ushetani ndio anakuja na message STRANGE ya madai, ameitafutia sababu na kuitengenezea ajenda kwa kuja na Deni la milioni 19, nitakuwa na wazimu kiasi gani mtu anaenidai milioni 19, ambae nina uhakika nina amana yake nimsumbue kwasababu ya LAPTOP, nimedai sababu NINAJIAMINI!! Na hapa ni kweli nina RB yake na ninamtafuta sababu anataka kudhulumu mali yangu tena kwa njia mbaya zaidi na kunichafua ili aendelee kukaa nayo, niliishi nae kwa Upendo mkubwa na kumuweka karibu bila kumuwekea mpaka wa mfanyakazi na Boss (Ndivyo ninavyoishi na wote)

MWISHO KABISA:

niliishi nae kwa Upendo mkubwa na kumuweka karibu bila kumuwekea mpaka wa mfanyakazi na Boss, kilichotokea alifeel ENTITLED na kuanza kukanyaga wengi, ni mtu wa mamlaka na kupenda kuamrisha watu muda wote, Kibri kupitiliza, hana heshima na wengine kiasi ilianza kujenga matabaka ofisini kwa kila mtu kuhisi nampendelea maana anafanya vitu wazi na sichukui hatua zaidi ya kuongea nae pembeni kumkanya, bila kusahau kujiweka juu na kuvunja nguvu wengine, na yote yameletwa na HOFU, hofu ya kuhisi kuna nafasi yake inachukuliwa ilimtawala baada ya watu kuongezeka kiasi cha kuharibu kazi nyingi, alikuwa ana uwezo hata ofisi kitu kisiende ili tu mtu mwingine ionekane hawezi, nimeona sio mtu ninaeweza kwenda nae safari moja, na NIMEMSIMAMISHA KUFIKA OFISINI!! Na ndio haya yote yametokea kaona solution ni KUNIKOMOA (he believes amenikomoa) which niseme tu ameishibisha nafsi yake, na ni kawaida yake maana hii sio mara ya kwanza kupeleka vitu vya ofisi hata confidential nje, alishafanya kwenye Clip ya Behind the Gram ambayo haijatoka akaichukua na kuipeleka alipopeleka hii hadithi yake leo, so nililitegemea hili hata wakati ninafanya maamuzi, japo sikutegemea kusukwasukwa uongo’ but tayari alishawapigia simu baadhi ya wenzie ofisini na kuwaambia anaenda huko alipoenda, na wameniambia!!

NASISITIZA HANIDAI CHOCHOTE ZAIDI YA MIMI KUMDAI LAPTOP AMBAYO ANAISUKIASUKIA UONGO AWEZE KUBAKI NAYO, NA HAKUNA MTU ANAEWEZA KUDAI SEHEMU MIAKA MIWILI AKAWA HIVYO ALIVYO YEYE, kiufupi HII HAITANIZUIA KUDAI CHA KWANGU, KESI ITAENDELEA NA SHERIA ITAAMUA.

 Nilichogundua watu wengi wanaumiza watu maarufu kwa njia ya kuweka mambo public, hata pale ambapo hawana makosa yatasukwa ya kusukwa na mtu mwenye sababu, wanadhani ndio hofu za wengi hivyo huitumia kama fimbo ili tu wawadhalilishe kwa uongo na kuwanyima uhuru wao, uhuru wangu uko pale pale, na Kesi iliyokuwepo ITAENDELEA, Yote kheri!!

Nimeliweka hili wazi kwa heshima ya watu ninaofanya nao kazi na si vinginevyo, SIJAWAHI KUMDHULUMU, SINA NIA YA KUMDHULUMU, SITAKAA NIMDHULUMU!! Hiyo ni hasira yake ya kumsimamisha kufika Ofisini na si vinginevyo.

Atakaeamini ataamini asieamini asiamini!! Nimemaliza










----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad