Mshambuliaji hatari wa Azam FC, Prince Dube anatarajia kuukosa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Dodoma Jiji FC utakaopigwa Oktoba 3 kutokana na kusumbuliwa na majereha ya nyama za paja.
Kwenye mchezo dhidi ya Singida Big Stars ambao Azam FC iliishinda kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja Chamazi jijini Dar es salam, Dube alipatwa na majeraha hayo.
Daktari wa Azam FC Dk Mbaruku Mlinga amesema kuwa, Dube alipata majeraha kwenye misuli ya paja na amepewa mapumziko ya juma moja baada ya hapo atafanyiwa vipimo tena.
“Dube atakuwa nje kwa juma moja na zaidi, baada ya hapo atafanyiwa vipimo tena hivyo ni wazi mchezo wa Ligi unaofuata hataweza kucheza hii ni kwa ajili ya kuangalia afya yake” amesema Dk Mbaruku na kuongeza;
“Kipimo cha kwanza kimebaini tatizo hilo, hivyo baada ya juma moja tutafanya kipimo kingine ambacho kitatoa majibu ya kuendelea kumtumia au aendelee na matibabu.”
Katika mechi tatu zilizopita za Ligi Kuu Bara, nyota huyo ameifungia Azam FC mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao alianza dhidi ya Tabora United iliyocheza pungufu na pia kuitungua Tanzania Prisons.
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA