Goli Tano Dhidi ya Simba Zamponza Msemaji Ally Kamwe wa Yanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Goli Tano Dhidi ya Simba Zamponza Msemaji Ally Kamwe wa Yanga

Afisa Habari wa Yanga SC Ally Kamwe amesema baba yake Mzee Shaban Ramadhani Kamwe bado ‘amemblock’ kufuatia matokea ya goli 5-1 ya watani wa jadi Yanga SC na Simba SC.

“Mzee wangu bado ameniblock, hataki kuwasiliana na mimi kwa njia ya mtandao, lakini naamini hapa kuna vyombo vikubwa vya habari, vyombo ambavyo iwe anataka au hataki atavifuatilia, na mimi pia nitumie jukwaa hili, kwa sababu ameniblock hatuwezi kuwasiliana..nimwambie mzee Shaban Ramadhani Kamwe..tabu bado iko palepale mzee…”.Afisa habari wa Yanga SC Ally Kamwe

Kamwe ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akifanyiwa mahojiano na vyombo vya habari nje ya Ukumbi wa bunge.

Katika hatua nyingine Ally Kamwe amesema kama Klabu ya Yanga wataendelea kusherehekea ushindi wa Goli 5-1 dhidi ya watani wao Simba SC kwa kuwa hawataki hii kumbukumbu ipotee na waendelee kukumbuka kwamba Novemba 05 watu walichukua tano.

“Tunataka tukisafiri kwenda Algeria,hapa Tanzania watu wasije wakasahau wajue kwamba novemba 05 kuna mtu alichukua tano, lakini tunataka pia vizazi vitakavyokuja,viwe na kumbukumbu… sisi kama yanga tunajua mwanzo wa sherehe lakini hatujui mwisho wake ni lini”.Afisa Habari wa Yanga SC Ally Kamwe

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad