Haji Manara Yamfika Hapa, Aandika Ujumbe Mzito Kwenda Kwa MANGE Kimambi ''Malipo ni Hapa Hapa Duniani''

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Haji Manara Yamfika Hapa, Aandika Ujumbe Mzito Kwenda Kwa MANGE Kimambi ''Malipo ni Hapa Hapa Duniani''


Ameandika Haji Manara:

Gazeti lako hili dada yangu kipenzi ngoja na mimi nitumie Mtandao huu huu ulionishauri Majuzi kuhusu aina ya Mke wangu ajae, kukushauri kwa upendo mkubwa nilionao kwako.


Vita zote za sasa unazopambana na kuwadhalilisha wenzio zingatia zina mwisho mbaya, hawajawahi Waja wengi kwa mpigo na kwa miaka mingi wakadhalilika wao tu, una zaidi ya Miaka kumi na Tano ni Mapambano tu ambayo mengi yamevunja hadi ndoa za Watu, Makazini wapo hata waliopoteza ajira, Ushaharibu sana Biashara za Watu, Ushawatukana hadi Viongozi wakubwa wa Nchi, tena matusi ya nguoni!!


Utetezi wako mkubwa ni kwamba wewe unaletewa habari, Yes lakini Lazima uzichuje kuepuka fedheha za Wenzio wenye Watoto kama wewe,Tambua hawa uliowadhalilisha nao wana Mungu na usidhani Mungu siku zote ataacha kusikia kiliio chao, lakini pia Story zako nyingi ni za kutunga kama ulivyotunga ya mimi na Tigo bila ushahidi wowote wa demand letter yako ya kubuni ( tunavyokujua ungeiweka Public )


Na hutunga Uongo ili App iwe active na huchukia sana kutokuwa wa kwanza kupata Story na hapo ndio hupata hasira za kutunga hata Uongo.


Uliniusia juzi na mimi nakuusia hapa hapa insta , App yako inaingiza maokoto lakini kuwa na kiasi, najua pia hupendi kuambiwa ukweli kwa kuwa umejipa Uungu flani hivi, ila ukiendelea malipo yake yanaweza kuja kuistua hii nchi kama c dunia.


Narudia sijakukataza na sikushauri uachane na App yako na umbea wako, lakini kiasi ni muhimu sana, leo hao hao wanaokushangilia wanasubiria yako Wakuulize kiko wapi? na wapo wengi kuliko unavyodhani.WATAKUSUUZA HASA


Najua Wabongo wengi hupenda Umbea na habari

za Watu,.lakini wewe kama Mzazi na Mwanamke uliyejaaliwa akili za kutosha, Tumia elimu ya kiasi na pia kataa uongo wa kuzusha, utafika mbali mno, najua pia ulivyotengeneza brand ya kuogopewa na Wabongo, Sio rahisi upewe ushauri huu hadharani,.ila pokea hiii MALIPO NI HAPA HAPA DUNIANI.


Nakuomba sana kama vile unavyoniomba mm juzi,umri wako na hiki unachoendelea kufanya ni mbingu na ardhi,.Fifty hiyo ishajongea na soon utajukuu!! Bad luck utatamani upate langu jipya baada ya huu ushauri,lakini level yangu ya kukupuuza ushaijua ilivyo!! Sijali muhimu nimeshakupa ushauri 🙏🙏

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad