Kauli ya Zuchu Baada ya Walimu Kushushwa Vyeo Kisa Wimbo Wake wa Honey

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Kauli ya Zuchu Baada ya Walimu Kushushwa Vyeo Kisa Wimbo Wake wa Honey

 Kauli ya Zuchu Baada ya Walimu Kushushwa Vyeo Kisa Wimbo Wake wa Honey

Msanii Zuchu hatimaye amevunja kimya chake ikiwa ni siku chache tu baada ya walimu wakuu wawili kushushwa vyeo vyao kufuatia klipu ya wanafunzi katika shule zao wakicheza densi ya wimbo wa Honey.


Mkoani Songwe, walimu wakuu wawili wa shule za msingi walipoteza vyeo vyao na kufanywa kuwa walimu wa kawaida tu kufuatia klipu hizo zilizosambaa watoto shuleni wakicheza densi ya wimbo huo.


Taarifa za awali zilidai kwamba waziri wa elimu katika taifa hilo alitoa amri ya wawili hao kushushwa vyeo mara moja kutokana na kukubali watoto kuchezewa nyimbo alizozitaja kuwa hazina maadili shuleni.


Baada ya habari hizo kusagaa kote mitandaoni, msanii Zuchu katika kipindi cha Jana na Leo kwenye Wasafi FM, alisema kwamba binafsi aliumia pakubwa kutokana na agizo hilo la wizara ya elimu kuwashusha vyeo walimu.

SOMA PIA: Kocha Robertinho Aguna Baada ya Bao TANO na Kuamua Kuwapongeza Yanga Kwa Mziki Waliochezeshwa

“Binafsi nimeumia kwa sababu walimu hao walikuwa wanapata mshahara mzuri lakini baada ya kushushwa cheo pengine hata maslahi yao yatapungua,” alisema kwa mahojiano ya njia ya simu na mtangazaji Baba Levo.


Msanii huyo pia alisisitiza kwamba yeye haoni shida yoyote kwa watoto kula burudani kwa kutumia iwmbo wake.


“Mimi sioni shida kwa sababu katika wimbo wangu mashairi yako sawa na sioni tatizo kwa watoto kuucheza wimbo wangu,” aliongeza.


Watoto hao walikuwa wanacheza wimbo huo baada tu ya kampuni moja kupeleka msaada katika eneo hilo na hili lilitokea baada ya kukamilika kwa hafla rasmi na kupisha kipindi cha burudani.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad