Mikoa Mitano iliyoathirika na Mvua Hadi Sasa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Mikoa Mitano iliyoathirika na Mvua Hadi Sasa

Mvua za El Nino zimesababisha athari kubwa katika miundombinu ya barabara na madaraja katika Mikoa ya Dar Es Salaam, Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Songwe.


Akitoa tathimini hiyo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara TANROAD nchini, Mhandisi Mohamed Besta wakati akiongea na waandishi wa habari mara baada ya ukaguzi wa kalavati kwenye eneo la Bwiko barabara kuu ya Mombo Same.


Amesema mikoa hiyo imepata athari kubwa kwa miundombinu ya barabara kuharibika, ikiwemo na madaraja kukatika hali ambayo imesababisha changamoto na athari kwa watumiaji wa barabara


"Mvua hii ambayo imenyesha kwa kiwango kikubwa imeleta athari lakini kwa kiwango kikubwa tumeweza kukarabati maeneo mengi ambayo yalikosa mawasiliano na sasa yanapitika"amesema Mhandisi Besta.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad