Papa Francis Amtimua Askofu Anayepinga Mabadiliko

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Papa Francis Amtimua Askofu Anayepinga Mabadiliko


Papa Francis Amtimua Askofu Anayepinga Mabadiliko

Papa Francis amemfuta kazi askofu Joseph Strickland, ambaye ni mkosoaji mkubwa ambaye ameibua maswali juu ya uongozi wa Papa katika Kanisa Katoliki.


Kwa mujibu wa taarifa ya Vatican, askofu huyo ameondolewa madarakani kufuatia uchunguzi katika Dayosisi ya Tyler, huko Texas, Marekani aliyokuwa akiiongoza.


Askofu Strickland ni mmoja kati sauti kinara katika tawi la uongozi wa Kanisa Katoliki nchini Marekani ambalo linapinga vikali mabadiliko yanayopigiwa chapuo na Papa.


Kuondolewa kwake kunakuja baada ya Papa kuzungumzia juu ya hali “ya kuwa nyuma” kifikra ya baadhi ya viongozi wa Kikatoliki nchini Marekani.


Askofu Strickland mara kadhaa ameshambulia hatua za Papa kutaka kubadili msimamo wa Ukatoliki katika masuala kadhaa ya kijamii ikiwemo kutoa mimba, haki za waliobadili jinsia na ndoa za jinsi moja.


Mwezi Julai mwaka huu, alionya kuwa mafunzo mengi ya Ukatoliki ambayo ni ya “ukweli wa msingi” yalikuwa yanapingwa, ikiwemo kile alichokiita majaribio ya “kudunisha” ndoa “kama ilivyoundwa na Mungu” baina ya mwanamume na mwanamke tu.


Askofu huyo pia amekosoa majaribio hayo aliyoyaita ya “kuvunja miiko” na kusema wanaoyapigia chapuo “wanapinga utambulisho wao wa kibailojia waliopewa na Mungu”.


Katika barua yake ya mwezi Julai, askofu Strickland amedai kuwa majaribio “kubadilisha visivyobadilika” yatasababisha mfarakano mkubwa ndani ya Kanisa. Na wale wanaotaka mabadiliko, ameonya kuwa “ndio hasa wanaofarakanisha [Kanisa]".


Askofu Strickland alikuwa chini ya uchunguzi wa Vatican na hapo awali alitupilia mbali uwezekano wa kujiuzulu, na katika barua ya wazi mwezi Septemba alimtaka Papa amfute kazi.


"Siwezi kujiuzulu kama Askofu wa Tyler kwa sababu kufanya hivyo itakuwa ninawatelekeza wana kondoo,” alisema.


Tunaendelea kukupa maelezo zaidi kuhusu taarifa hii.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad