Paul Makonda "Mawaziri Mtawasilisha Ripoti Kazi Mlizofanya"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Paul Makonda "Mawaziri Mtawasilisha Ripoti Kazi Mlizofanya"

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewataka Mawaziri wote kila robo ya mwaka ya kibajeti kuandaa taarifa na kuiwasilisha kwenye Sekretarieti ya CCM Taifa ikielezea utekelezaji wa kazi waliyopewa na Serikali na kwamba Waziri ambaye hatofanya hivyo atachukuliwa hatua.

Akiongea leo Dodoma, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi CCM, Paul Makonda @baba_keagan amesema “Kutokana na msingi wa Dkt. Samia kuweka bajeti kubwa ya kuwapigania na kuwaletea maendeleo Wananchi, Chama kinawataka Mawaziri wote kila robo ya mwaka ya kibajeti kuandaa taarifa na kuiwasilisha kwenye Sekretarieti ya Chama Taifa ikielezea utekelezaji wa kazi waliyopewa na Serikali”

“Kazi hii wamepewa na Mwenyekiti wetu wa Chama, Chama kinataka kupata ripoti kila robo ya Chama wamefanya nini?, na Waziri yeyote ambaye atakaa ndani ya robo ya mwaka hajafanya kazi , hana ripoti, hakuna utekelezaji wa Ilani, Chama hakitosita kumchukulia hatua kwani sasa ni wakati wa kufunga mkanda kuwatumikia Wananchi”

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad