PAUL Makonda "Mnaolipa Watu Watukane Viongozi Nawajua"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

PAUL Makonda "Mnaolipa Watu Watukane Viongozi Nawajua"


Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi CCM, Paul Makonda @baba_keagan amesema kuna baadhi ya Watu wanawalipa Watu pesa ili wawatukane Viongozi mitandaoni ambapo amesema anawafahamu Watu hao na kama aliweza kuwataja wauza unga hashindwi kuwataja na wao pia.

“Tuna wajibu wa kuliombea Taifa na kuwaombea Viongozi wetu, wasiolitakia mema Taifa letu watamnenea mabaya Rais wetu na mnaona wengine wanalipa Watu mitandoni na bahati mbaya Mimi mdogo wao nawajua, Mimi nikikaa nikiangalia kwenye mtandao wale wenye majina makubwa najua huu mwandiko wa fulani, si nimelelewa na hawa Wazee hawa nimekaa chini ya akina Sitta, Membe, Magufuli wamenilea, nikikaa niangalia hivi nasema mmh, sasa Mimi siwachukii wale wanaondika kwasababu wanalipwa nao wanapata ugali ndio maana huwezi sikia nakuwa na tatizo na anayeniandika vibaya lakini sio kumwandika Rais vibaya”


“Na wengine wanaowalipa wanaoandika vibaya kwenye mitandao ni wale wanaolipwa mshahara na Dkt. Samia (Ambaye nae wanamtukana) mnanifahamu, mnanijua, kama Wauza unga niliwasema sembuse hawa wanaomtukana Rais , niseme tu Kaka zangu acheni, muacheni Rais afanye kazi, Mwacheni Mwenyekiti wa Chama afanye kazi, nyie kazi yenu moja kumuombea , la pili kumshauri , usitaka afanye kile unachotaka wewe tu ndio kizuri, Taifa hili lina Watu wengi”


“Acheni kuwachafua Makamu wetu Mwenyekiti wa Chama Taifa bara, acheni kumchafua Dr. Mwinyi, acheni kumchafua Katibu Mkuu wetu Chongolo, tuwape nafasi Viongozi wetu wafanye kazi, nawafahamu na miandiko yenu naijua na hata mnazowatumia najua , Mimi najua nilipotolewa na Mungu”

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad