Upepo wa Diamond Platnumz Wamsaidia Juma Jux Kuvunja Rekodi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Upepo wa Diamond Platnumz Wamsaidia Juma Jux Kuvunja Rekodi


Kwenye orodha ya nyimbo 10 za 2023 tulizozitabiria kuvuka mwaka hata kufanya vizuri mwanzoni mwa mwaka 2024, wimbo wa Jux na Diamond Platnumz ‘Enjoy’ ndio tuliupa namba moja.


Kasi ya ukuaji wake katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, ilitumika kama kigezo kikubwa kilichothibitisha wimbo huo unaweza kuwa miongoni mwa nyimbo za 2023, zitakazosikilizwa mara nyingi hadi mwaka 2024.


Video hiyo ambayo ilikuwa Premiered Agosti 7 mwaka huu, inaonekana kuwa miongoni mwa video za Bongo fleva zinazokua kwa kasi kubwa, tukilinganisha na nyimbo zote zilizoachiwa katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.


Ikiwa na zaidi ya watazamaji milioni 32 YouTube, video ya wimbo huo imevunja rekodi ya Jux; ikiwa ni video yake ya kwanza kufikisha watazamaji milioni 30, ikifuatiwa na ‘Sugua’ Feat. Diamond Platnumz ya mwaka 2020 ambayo ina watazamji milioni 12.


Kolabo na Diamond Platnumz zinaonyesha kuwa ni muunganiko mzuri, kila wakati ambao Jux anamvuta Diamond Platnumz studio, mambo huwa supa. Tutaikumbuka ‘Sugua’ kama mojawapo ya nyimbo zilizovuma sana hata kuwepo kwenye kundi la nyimbo zilizofanya vizuri kipindi hicho.


Video ya kwanza kupandishwa kwenye YouTube Chaneli ya Jux, ilichapishwa Julai 15, 2015. Video hiyo ambayo ni kichupa cha wimbo wake ‘Nikuite Nani,’ imekusanya zaidi ya watazamaji milioni 1.3 katika kipindi cha miaka nane iliyopita.


Tunaweza kuona ugumu wa safari ya Jux katika kuutafuta ukubwa wake YouTube. Miaka yake nane YouTube amefanikiwa kuchapisha video zaidi ya 200 huku akikusanya zaidi ya subscribers 991,000.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad