Header Ads Widget


Yanga, Simba kukipiga siku moja Klabu Bingwa

Yanga, Simba kukipiga siku moja Klabu Bingwa


Wakati mzunguko wa kwanza wa Hatua ya Makundi ukianza kwa vilabu vya Yanga na Simba kucheza kwa siku tofauti, mechi zao za pili vilabu hivyo vikongwe nchini vitakipiga siku moja.


Yanga anatarajia kuianza kampeni yake ya kutoboa Makundi ya Klabu Bingwa hapo kesho Novemba 24, 2023 ugenini dhidi ya CR Belouzdad huku Simba akicheza nyumbani kesho kutwa Jumapili dhidi ya ASEC Mimosas.


Mechi zao za pili zitapigwa Desemba 2, 2023 ambapo Simba atakuwa ugenini dhidi ya Jwaneng Galaxy majira ya saa 10:00 jioni huku Yanga akimkaribisha nyumbani Al Ahly siku hiyohiyo majira ya saa 1:00 usiku.

Post a Comment

0 Comments