Ally Kamwe Awajia Juu Wachambuzi Kisa Kutozungumzia Uwezo wa Aziz K Msimu Huu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Ally Kamwe Awajia Juu Wachambuzi Kisa Kutozungumzia Uwezo wa Aziz K Msimu Huu

Msemaji wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amehoji kuhusu wachambuzi kutozungunzia uwezo wa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Stephane Aziz Ki ambaye mpaka sasa ndiye kinara wa upachikaji mabao kwenye Ligi Kuu akiwa na mabao 9 wakati wanaomfuatia wana mabao 7 kila mmoja.

Aziz Ki ambaye ni raia wa Ivory Coast amekuwa na mwendelezo mzuri msimu huu tofauti na msimu uliopita aliposajiliwa Jangwani akitokea Asec Mimosas ya nchini humo.

Kamwe amesema kuwa, iwapo tu Aziz Ki anafunga vile, vipi kama klabu hiyo ikasajili mshambuliaji wa hatari, mabao ya Yanga yatakuwa zaidi ya hayo yanayofungwa sasa.

“Watu hawamzungumzi kuhusu Aziz Ki, kama hafanyi kitu hivi maana kafunga magoli 9 kwenye michezo 10 maana mfungaji bora wa msimu uliopita alikuwa na magoli 17 lakini watu wapo kimya kabisa na bado kuna kelele kwamba Yanga haina mshmbuliaji lakini mfungaji kinara wa magoli kwa sasa yupo Yanga, Je tukileta mfungaji mpya watu si watakuja kufa?

“Mnahesabu lakini? Mechi 10, goli 9… top scorer wa ligi mpaka sasa… Stephane Aziz Ki. Wachambuzi mko kimya sana kuhusu Aziz Ki, hatujawazoea hivyo,” amesema Kamwe.

Msimu uliopita Aziz Ki katika mechi 30 za NBC Priemer League

9 Goals

4 Assits

Aziz Ki msimu huu katika mechi 10 za NBC Priemer League.

9 Goals

3 Assits.

⚽ WAFUNGAJI WA YANGA SC 2023/2024 NBC PL MSIMU HUU

1. Stephen Aziz Ki -9

2. Max Zengeli -7

3. Pacome Zouzoua – 4

4. Kennedy Musonda – 3

5. Mudathir Yahya -2

6. Dickson Job -1

7. Hafiz Konkoni -1

8. Yao Attohoula -1

9. Clement Mzize -1

10. Skudu Makudubela -1

MAGOLI YA KUFUNGA – 30

MAGOLI YA KUFUNGWA – 6

Unadhani Aziz Ki atachukua kiatu cha ufungaji Bora msimu huu?

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad