Ifahamu Historia ya ‘Boxing Day’

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Ifahamu Historia ya ‘Boxing Day’

Kila ifikapo Desemba 26, dunia husherehekea sikukuu ya ‘boxing day’ ambayo mara nyingi huenda sambamba na kutoa na kupokea zawadi.


Hii ni siku ya pili baada ya kusherehekea sikukuu ya Krismasi. Zaidi ya Sh22.7 trilioni zinatarajiwa kutumika duniani mwaka huu katika manunuzi ya zawadi za siku hiyo kwa mujibu wa mtandao wa ‘The Sydney Morning Gerlad’ wa nchini Australia.


Matumizi hayo yatakuwa ni ongezeko la asilimia 1.6 ya matumizi yaliyofanyika katika kipindi kama hicho mwaka 2022. Utafiti huo unaonyesha katika bidhaa zitakazoongoza kununuliwa zaidi ni vifaa vya kazi, nguo, vyakula na mapambo.


Historia ya ‘boxing day’


Tovuti ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) inasema ‘Boxing Day’ ilianza kuitwa hivyo wakati Malkia Victoria wa Uingereza akiwa madarakani mwaka 1800, kutokana na utamaduni uliokuwapo wakati huo uliohusisha familia za kitajiri kutoa zawadi kwa familia za kimasikini.


“Kwa kuwa watumishi wa watu wa tabaka la juu walitakiwa kufanya kazi siku ya Krismasi, hivyo siku iliyofuata waajiri waliwapatia wafanyakazi masanduku yenye zawadi, fedha na mabaki ya Krismasi kama vile bonasi ya likizo,” imeandika tovuti hiyo katika moja ya makala yake iliyoelezea asili ya sikukuu ya boxing day.


Hata hivyo, tovuti ya www.history.com inaeleza nadharia nyingine kuhusu asili ya sikukuu hiyo ya kupeana zawadi, “Jina la ‘boxing day’ lilitokana na masanduku ya sadaka yaliyowekwa makanisani kwa ajili ya kukusanya michango kwa wale wanaohitaji, kisha Desemba 26 makasisi hutoa fedha hizo kwa masikini kwa heshima ya sikukuu ya Mtakatifu Stefano, shahidi Mkristo anayejulikana kwa matendo ya hisani,” imeeleza tovuti hiyo.


Wachumi waielezea


Mack Patrick, ambaye ni mchumi anasema sikukuu ya hiyo pamoja na nyingine za mwishoni mwa mwaka zinachochea ukuaji na ongezeko la biashara duniani na nchini pia.


“Katika kitu ambacho nchi za Ulaya kinanufaika nacho katika kujiimarisha kiuchumi ni sikukuu za mwishoni mwa mwaka, kwao huo ni muda wa manunuzi hasa na hii inasababisha mzunguko wa fedha kuongezeka,” amesema.


Alisema, “Kumbuka biashara zinapofanyika pia Serikali inapata kodi ambayo itatumika kutekeleza miradi mingine ya maendeleo.


Kuhusu boxing day, Patrick alisema bado Tanzania inashindwa kutumia vizuri sherehe hiyo katika upande wa biashara. “Bado hatuna tabia ya manunuzi katika kipindi hiki japokuwa ukienda baadhi ya maeneo kama vile Moshi, kule biashara inafanyika hasa na katika nyakati hizi watakuwa wanakusanya sana kodi,” amesema.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad