Aliyemuomba Rais Samia Cherehani Apewa Nne

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemnunulia cherehani nne, Beatrice Mwalingo (28) ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa kwake siku tisa zilizopita.

Januari 25, 2024 kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, Rais Samia alitoa ahadi kwa binti huyo, baada ya kuomba zawadi akitoka nchini Indonesia.

Katika chapisho la Rais Samia siku hiyo, alikuwa akielezea juu ya kuwasili kwake nchini Indonesia kwa ziara ya kitaifa ya siku tatu kufuatia mwaliko wa Rais wa nchi hiyo.

“Uhusiano wa Tanzania na Indonesia ambao mapema mwezi huu (Januari 13) ulitimiza miaka 59, umekuwa wenye tija kwa nchi yetu na mamilioni ya Watanzania hasa kwenye kilimo na biashara. Tunaendelea kuifanya kazi ya kukuza uhusiano huu, ili kuleta tija zaidi kiuchumi kwa nchi yetu,” aliandika Rais.

Hata hivyo, Beatrice bila kujua itakuwa siku yake ya bahati, aliacha ujumbe chini ya chapisho hilo uliosomeka. “Sawa mama. Ukiwa unarudi nyumbani naomba uniletee zawadi ya cherehani.”

Muda mchache baadaye, Rais Samia alijibu ujumbe wake na kumuambia. “Hujambo, Beatrice? Nimepata wasaa wa kuusoma ujumbe wako. Hongera kwa kazi na kujituma.

Wasaidizi wangu watawasiliana na wewe kukusaidia upate mashine uliyoomba kwa shughuli zako. Nakutakia kila la kheri.”

Hatimaye jana Jumamosi, Januari 3, 2024, ilikuwa siku nyingine ya furaha kwa Beatrice baada ya kupewa zaidi ya kile alichokiomba.


"Nimefurahi sana zawadi aliyonipatia kiukweli itanisaidia katika shughuli zangu za kila siku, kati ya cherehani nne nilizopewa, mbili sikuwa nazo kabisa. Kupitia zawadi hii nimeongeza ajira za watu wanne," amesema Beatrice alipozungumza na Mwananchi Digital.

Amesema alipopewa ahadi hiyo alihisi kama ni ndoto na kusubiri mpaka pale ilipotekelezwa.

"Niwasihi tu vijana wenzangu kutumia vizuri mitandao isiwe sehemu ya kumalizia hasira zetu, bali iwe sehemu ya fursa, tuangalie nini nini cha kuandika hata kama umekwazika ni vyema kuangalia namna ya kufikisha ujumbe," amesema Beatrice.

Wadau waibuka kwenye Instagram yake


Leo baada ya kuchapisha kipande hicho cha video kwenye Instagram yake kama ilivyo ada wamejitokeza wadau mbalimbali kumpongeza na wengine kumtania.

“ukumbuke kumshonea na mama @samia_suluhu_hassan nguo kama zawadi ya shukrani @beatrice_only1 Asante” huyu ni iam Rickson.

Mwingine yassin_husse93 amesema “Sasa na wewe toa moja tuone kama una moyo wa kutoa naiomba mimi”, Naye jackie.f.k “Hongera sana dada, ungemshonea mama japo gauni ingekuwa vizuri zaidi aone jinsi cherehani alizokupa zinapiga kazi”

meca_beautyproduct “Hizo cherehani ni za wananchi wote, tutakuja na vitambaa na uzi wetu tushone na tuondoke”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad