Kwa Mara ya Kwanza Rais wa Zanzibar Afunguka Sakata la Waziri Wake Kujiuzulu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Rais wa Zanzibar, Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema Kiongozi akitaka kujiuzulu anapaswa kumpa taarifa Boss wake kwanza badala ya kukurupuka kwenda kutangaza kwenye Vyombo vya Habari huku akitoboa siri kuwa hata yeye akiwa Waziri wa Ulinzi aliwahi kumwandikia barua ya kujiuzulu Rais Mstaafu Kikwete baada ya mabomu ya Gongolamboto lakini alimwambia ile ni ajali na hana sababu ya kijiuzulu.

Akiongea leo February 1, 2024 wakati akiwaapisha Mawaziri wapya wateule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ikulu Zanzibar Rais Mwinyi amesema “Suala la kujiuzulu Waziri ni suala ambalo si geni ni moja katika njia ya kuwajibika, katika Wizara kunaweza kukawa na mazingira mawili ya Waziri kujiuzulu, mazingira ya kwanza yanaweza kuwa katika Sekta yako inayoisimamia kumetokea tatizo au changamoto na wewe kama Waziri unawajibika kwa changamoto ile, si lazima uwe umeifanya wewe lakini unawajibika kwasababu wewe ndio Msimamizi wa Sekta”

“Nimekuwa nasikia kwenye mitandao kuwa Zanzibar hajawahi kujiuzulu Mtu, si kweli, wakati wa ajali ya meli kuna Waziri alijiuzulu na alijiuzulu si kwasababu alisababisha
yeye ile ajali kawajibika kwasababu ni Sekta anayoisimamia na kilichotokea ilikuwa ni uzembe na si ajali”

“Ilipotokea ajali ya mabomu kule gongo la mboto, Mimi nikiwa Waziri wa ulinzi nilipeleka ujumbe kwa Rais wangu wakati huo Mhe.Kikwete nikimtaka aliridhie nijiuzulu lakini sikukurupuka kwenda kwenye Vyombo vya Habari nikatangaza kwamba nimejiuzulu sio utaratibu, utaratibu unataka umwambie aliyekuteua akubali ndio ukatangaze kujiuzulu, Mhe.Kikwete akasema hii ni ajali huna sababu ya kujiuzulu, hakuna Mtu aliyesikia kama nilitaka kujiuzulu leo nasema hili hadharani lakini sikuwahi kulisema”

Kauli ya Rais Mwinyi inakuja siku chache baada ya aliyekuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Simai Mohammed Said, kujitokeza kwenye Vyombo vya Habari na kutangaza kujiuzulu nafasi yake ya Uwaziri akisema mazingira ya kutekeleza jukumu hilo yamekuwa magumu. #MillardAyoUPDATES
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad