Tanzania kupeleka waamuzi AFCON

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Shirikisho la Soka ‘TFF’ limesema Tanzania itakuwa kituo cha mafunzo ya mfumno wa VAR kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ‘CECAFA’.


Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred amesema kutokana na hilo wameanza kupata waamuzi watakaochezesha michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON’.


“Kama nchi huwezi kutengeneza waamuzi wote bora, ila unaweza kupata waamuzi wanne ambao watakuwa wanawakilisha, hata huko Sudan hawaendi wote, ni wawili au watatu bora. Tumeanza kuona mafanikio kwani tumepata waamuzi ambao wameanza kuingizwa kwenye mchakato wa AFCON 2025.


“Kwa hiyo kuna kazi kubwa imeanza kufanyika kwa waamuzi wa kiume na wanawake. Jitihada nyingi zimefanyika kuwasaidia ikiwemo ujio wa mitambo miwili ya VAR, mmoja utakuwa Benjamin Mkapa na mwingine utakuwa unahamahama,” amesema Kidao.


Kuhusu Tanzania kutokuwa na waamuzi kwenye mashindano makubwa, Kidao amesema mwonekano wa mwamuzi, lugha ndio vitu vinavyofanya kukosa sifa na kuongeza kuwa wamekuja na mpango wa waamuzi vijana wenye vipaji ili kuondoa tatizo hilo.


Katika hatua nyingine, Kidao amesema Kamati ya Utendaji ya TFF itapitia taarifa ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche ya mashindano ya AFCON 2023 pamoja na ya Mkuu wa Msafara ambaye ni Rais wa Shirikisho la Soka Zanzibar ‘ZFF’, Dk Suleiman Jabir baada ya Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ kutoa majibu ya rufaa yake.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad