Geremi Njitap Mchezaji wa Cameroon Abaini Watoto Aliowalea Miaka 16 si Wake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Ndoa ya Nyota wa zamani wa Chelsea na timu ya Taifa ya Cameroon, #GeremiNjitap ipo katika mchakato wa talaka baada ya kubainika Watoto Mapacha waliozaliwa Mwaka 2008 miaka minne kabla ya kufunga ndoa na mkewe, Toukam Fotso Laure Verline si wake Kibaiolojia

Geremi (45) amefungua kesi Mahakamani akitaka ndoa ivunjike baada ya Vipimo vya Vinasaba (DNA) kuonesha Mapacha hao ambao mkewe alimuaminisha ni wa kwake, ni wa mwenza wa zamani wa Toukam

Nyaraka zilizovuja Mtandaoni zimeonesha Geremi amelalamika kukosewa heshima na mkewe ambaye alikuwa akimtolea lugha ya dharau mbele ya Watoto hao pia walikuwa na migogoro ya mara kwa mara

Geremi akiwa Beki wa Kulia mwenye uwezo wa kucheza nafasi ya Kiiungo Mkabaji alicheza pia katika Timu za Real Madrid, Middlesbrough na Newcastle United
-
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad