Huyu Hapa Ndio Mwanamke Chanzo Cha Unguko Kubwa la P Diddy

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Huyu Hapa Ndio Mwanamke Chanzo Cha Unguko Kubwa la P Diddy
Cassie and P Diddy

Habari kubwa duniani hivi sasa ni nyumba za rapper na mfanyabiashara mkubwa kwenye kiwanda cha muziki nchini Marekani Sean Love Combs maarufu kama P DIDDY zilizoko Miami na Los Angeles kufanyiwa uchunguzi na HSI(Homeland Security Investigation) pamoja na Law enforcement officers wengine.

Sababu kubwa inayohisiwa ni madai yanayomkabili Diddy ya unyanyasaji wa kijinsia,biashara ya ngono e.tc ambayo mwishoni mwa mwaka 2023 alishtakiwa na msanii wake wa zamani chini ya label yake ya Bad boy record label Cassandra Ventura maarufu kama @cassie mahakamani huko Manhattan.

@cassie na Diddy inadaiwa walikua kwenye mahusiano ya kimapenzi kuanzia mwaka 2007 na mwaka 2018 walidaiwa kuachana,mrembo huyo mwezi November 2023 alidai kuwa alipitia unyanyasaji kwa miaka mingi kutoka kwa Diddy kuanzia mwaka 2005 alipokutana na nguli huyo wa muziki wa Hip hop nchini humo na yeye alikua na miaka 19 tu.

@cassie alidai kuwa Diddy alikua akimpiga mara kwa mara na kuna wakati alifikia hatua ya kumpiga teke usoni na baadaye mwaka 2018 alimbaka,Cassie aliongeza na kusema kuwa alimsafirisha na kumshurutisha kufanya mapenzi na wafanyabiashara wa ngono kwenye miji tofauti huku yeye akichukua picha na kujichua.

Madai mengine dhidi ya Diddy ni ya mwanadada Joie Dickerson ambaye alidai Diddy alimuwekea madawa na kumfanyia unyanyasaji wa kingono kisha kurekodi,mwingine ni producer Rodney(Lil Rod) pamoja na wengine wawili.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad