Yanga Vs Mamelod Ndio Mechi Kubwa Inayozungumzwa Sana Afrika Nzima

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Yanga Vs Mamelod Ndio Mechi Kubwa Inayozungumzwa Sana Afrika Nzima
Yanga Vs Mamelodi

Inazungumzwa zaidi. Inachambuliwa zaidi. Tena na mataifa ya nje, ambao siyo Watanzania. Na pia inasubiriwa kwa hamu ndani na nje ya Tanzania.


Kifupi ndo 'BIGI MECHI' kwa sasa Afrika nzima. Kutokana na namna inavyoongolewa, kusubiriwa, kujadiliwa na hata timu husika zinavyojiandaa.

Mamelodi wameshatua Bongo. Wakati Al Ahly ambao watacheza kabla yao na Simba, bado hawajatua. Na Misri ni mbali kuliko Afrika Kusini.

Kwa maana hiyo hata Mamelodi wamepata hofu. Hawana uhakika na matokeo yao kwa Mkapa. Huku Yanga nao wakifanya kila njia kuona nyota wao wote wanakuwepo siku ya Jumamosi.

Kulifanyika mechi kubwa kama Simba na Al Ahly uzinduzi wa African Football League. Simba na Wydad robo fainali ya Klabu Bingwa msimu wa jana. Na hata Yanga na Belouzidad kupambania kuingia robo.

Lakini mechi ya Yanga na Mamelodi itakuwa kubwa kuliko. Haijawahi kutokea mechi kubwa ya klabu ya kiwango kama hiki. Hii ni zaidi ya mechi. Zaidi ya tukio na zaidi ya msisimko.

Mamelodi wametepeta kabla ya muda kuwadia.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad