Mbunge Ole Sendeka afunguka alivyofyatuliwa risasi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Mbunge Ole Sendeka afunguka alivyofyatuliwa risasi

Watu wasiojulikana wamemfyatulia risasi zisizopungua nne Mbunge wa Simanjiro (CCM) Mkoani Manyara, Christopher Ole-Sendeka akiwa ndani ya gari lake safarini na Dereva wake majira ya saa moja usiku wa jana Machi 29, 2024 na kisha kukimbia muda mfupi baada ya Mbunge huyo kuanza kupiga risasi juu kuwatishia.


Akiongea nasi kwa njia ya simu, Sendeka amesema; "Ni kweli nimeshambuliwa kwa risasi majira ya saa moja kasoro katika Wilaya ya Kiteto kati ya Kiji cha Ngabolo na Ndedo.


"Kulikuwa na gari ambayo ilikuwa inanifuatilia kwa nyuma tukawapisha kidogo kama tunataka kuwapisha wapite kulia walipofika usawa wetu wakaanza kumimina risasi kwa Dereva na baada ya hapo wakavuta kwenda mbele halafu wakaanza kuzipiga za usoni na sisi tukakata kona kugeuza na Mimi nikaanza kupigapiga (risasi) za juu pale kuwatishiatishia ndio tukafanikiwa kugeuza na kuondoka.


"Walikua na silaha kubwa na silaha ndogo, hakuna aliyepata madhara tulikuwa Mimi na Dereva wangu ni gari tu ndio wameichakazachakaza wameipigapiga, mpaka sasa kwakuwa tumekuja gizani huku hatujazihesabu lakini zipo risasi moja, mbili, tatu, nne kama nne hivi hatujazihesabu lakini nne au tano hivi zipo waziwazi (matundu ya risasi yanaonekana kwenye gari)"


"Kuhusu kwanini nimeshambuliwa bado sijui bado siwezi kusema jambo kwa wakati huu, sio rahisi pia kujua sura za waliohusika katika kipindi kama hicho" Mbunge Ole-Sendeka amesema.


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Lucas Mwakatundu akizungumza na nasi amesema tukio hilo limetokea jioni ya jana ljumaa Machi 29, katika eneo la Ndaleta, wilayani Kiteto wakati Ole Sendeka akiwa na dereva wake akielekea jimboni kwake Simanjiro.


"Ole Sendeka akiwa na dereva wake, gari lao lilishambuliwa kwa risasi ila hawakudhurika ni wazima kabisa," amesema Kaimu Kamanda Mwakatundu. Amesema polisi wanaendelea na uchunguzi na hakuna anayeshikiliwa kutokana na tukio hilo.


Kaimu Kamanda amesema kwa sasa Ole Sendeka na dereva wake walikwenda Kituo cha Polisi Kiteto wakiendelea kuhojiwa kuhusu tukio hilo. Fuatilia mitandao yetu kwa taarifa zaidi.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad