Ally Kamwe: Simba ni Timu TISHIO, Ina Viongozi Makini, Tusiidharau Tarehe 20

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ally Kamwe: Simba ni timu tishio, ina viongozi makini, Tusiidharau Tarehe 20


Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa wao kama Yanga wanaichukulia Simba SC kama timu tishio kwenye Ligi ya Tanzania na timu za Afrika Mashariki na Kati kutokana na ubora wao.


Kamwe amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari na kuelezea Mipango ya Timu yake kuelekea katika Mchezo wa Derby ya Kariakoo Dhidi ya Simba SC Mchezo ambao utachezwa Aprili 20 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.


“Hii mechi mpaka imekuwa dabi maan yake ina upekee wake, umuhimu wake na ugumu wake. Unapokwenda kwenye Dabi ya Kariakoo kwa mawazo ya kwamba umeshinda mechi nyingi, mshindani wangu ana hali mbaya, utaingia chaka.


“Sisi kama Yanga hatuitazami Simba kama mnavyoitazama, sisi tunaitazama Simba kama timu tishio (giant) tunayowania nayo ubingwa kwa sababu wana nafasi ya kutwaa ubingwa. Simba ni timu yenye wachezaji wazoefu waliocheza mechi nyingi kubwa na tunaitazama Simba kama timu yenye viongozi makini.


“Ukiniambia nitaje timu zenye viongozi makini siwezi kuiacha Simba, wana viongozi wazoefu na wanajua mipango ya kupata matokeo kwenye mechi ngumu licha ya kwamba wanapitia wakati mgumu lakini wapo imara.


“Simba wanweza kusumbuka kwenye mechi ndogo lakini ikija suala la mechi kubwa, mentality inabadilika, wanacheza kwa intensity ya juu," amesema Kamwe.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad