Bosi Yanga: Simba lazima watoe alama tatu, idadi ya mabao tutajua hukohuko

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Bosi Yanga: Simba lazima watoe alama tatu, idadi ya mabao tutajua hukohuko


Baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam kutokea Mwaza katika pambano lao dhidi ya Singida Fountain Gate, Mjumbe wa Kamati wa Utendaji Klabu ya Yanga, Alex Ngai ameuzungumzia mchezo wao ujao dhidi ya watani zao Simba SC.


Yanga watavaana na Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Jumamosi ijayo, Aprili 20, katika Dimba la Mkapa huku Yanga wakiwa na kumbukumbu ya kuifunga Simba mabao 5-1 karika duru ya kwanza.


“Tuna timu bora na tuna kikosi bora hatuna kitu kingine zaidi ya ubora tunahitaji kupata alama tatu tu idadi ya magoli hatujui lakini alama tatu lazima watuachie.


“Hakuna dabi nyepesi, dabi ya Simba na Yanga siku zote ni ngumu lakini tunaamini tutapata ushindi. Hakuna kitu kingine tunachojivunia zaidi ya kuwa na timu bora ili ushinde. Tunaamini katika kucheza mpira uwanjani, mazoezi na maandalizi mazuri," amesema Ngai

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad