Fiston Mayele Afunguka "Nilipoenda Kusajiliwa na Pyramids Nilivimba Mguu Hadi Leo"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mchezaji wa Zamani wa Yanga na Sasa Pyramids Fiston Mayele ameeleza kuwa alipitia hali ngumu sana Kimwili na Kisaikolojia, kwani kabla ya kwenda kusaini mkataba katika klabu ya Pyramids ya Misri Mguu wake ulianza kuvimba na kumuuma mno.

Akawa anatembelea magongo, analala sebuleni kwani alikuwa hawezi kupanda ngazi za chumbani kwake, anaongeshwa na kufanyiwa kila kitu na mkewe, na mguu ulikuwa hatarini kukatwa kama ungeoza, hali hii ilimfanya kuona kuwa hataweza kucheza mpira tena katika maisha yake akawa akawa analia usiku na mchana.

Muda huo Pryamids walikuwa wakimuita aende kusaini mkataba hali iliyomfanya kuwadanganya kuwa amefiwa ili avute muda hadi apate nafuu, ikambidi aende kwao Congo ndipo akapata nafuu akaenda kusaini mkataba na siku tatu mbele Pyramids walipo-post picha yake kwenye mtandao wao ya kijamii, mguu ukavimba tena na kuanza kumuuma mno.

Akarudi Tanzania na kwenda kuombewa kwa Mchungaji Mwamposa na akapata nafuu, na sasa anacheza hivohivo huku mguu ukiwa umevimba lakini kwa sasa hauna maumivu, huku akisisitiza kuwa mwisho wa msimu huu ataogea kila kitu.

Mayele amefunguka hayo katika kipindi cha Wednesday Night cha Azam TV.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad