KUMEKUCHA: Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha Adaiwa Kuomba Kuondoka Simba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


KUMEKUCHA: Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha Adaiwa Kuomba Kuondoka Simba
Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha


IMEELEZWA kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha huenda msimu ujao asiwepo kwenye benchi la ufundi la Wekundu hao wa Msimbazi baada ya kupata ofa ya kuinoa timu ya Taifa ya Algeria.

Taarifa za ndani ambazo bado hazijathibitishwa mapema zimesema kwamba, Benchikha tayari amewasilisha barua ya kuomba kuondoka katika Klabu hiyo.

Kwa mujibu wa tarifa hizo, Benchikha ameutaka uongozi kutoendelea kukinoa kikosi cha Simba kwa msimu ujao na kwa ajili ya kwenda kutafuta changamoto nyingine likiwemo dili hilo ambalo lipo mezani

Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, uongozi umeridhia maombi yake licha ya Mwekezaji, Mohammed Dewji (Mo) kutaka kuendelea na Benchikha kwa msimu mwingine.

“Suala la Benchikha kubaki kwa msimu ujao limekuwa gumu licha ya maombi ya mwekezaji na tayari mchakato wa kupata kocha mpya umeanza mapema,” amesema mtoa habari wetu.

Ameongeza: “Msimu wa 2024/25 anakuja kocha mwingine, Benchikha anaondoka na inadaiwa kwamba anawaniwa na timu ya taifa ya Algeria,” amesema mtoa habari huyo.

Ameongeza kuwa mchakato kumpa mrithi wa Benchikha utaanza mapema ili atakapoondoka kocha huyo wawe tayari na mtu wa kumtambulisha.


Alipoulizwa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally kuhusuiana na suala la Benchikha, amesema, “Sifahamu suala lolote kuhusu suala la kuondoka kwa Benchikha, ninachojua kwamba yeye ni kocha wetu, kikubwa tunapambana kuhakikisha tunashinda mechi zetu zote zilizobaki,” amesema Ahmed.

Wakati huo huo, mtoa habari huyo amesema kwa sasa mchezaji yeyote wakitaka kumsajili lazima wajumbe ambao wako kwenye kamati ya kumshauri Dewji (hawakupenda kuyataja majina yake) waende nae kwake kwa ajili ya kusaini mkataba.

Ameeleza kuwa wameanza kufanya kazi kimya kimya likiwemo suala la kocha mpya pamoja na kuwa kwenye program mpya kwa ajili ya kusaka wachezaji kwa ajili ya usajili kwa msimu ujao.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad