Paul Makonda : Wauza Unga Walitaka Kununua Kwa Drone Wakashindwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Paul Makonda : Wauza Unga Walitaka Kununua Kwa Drone Wakashindwa

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amewataka Polisi Mkoani Arusha kuachana na rushwa wanapotimiza majukumu yao ikiwemo ya udhibiti wa dawa za kulevya ambapo ametolea mfano wa namna alivyopambana na Wauza unga akiwa Dar es salaam hadi wengine kupanga njama za kumuua.

Akiongea na Maafisa wa Polisi leo April 20,2024, Makonda amesema “Ni vema Askari wote tukaweka kauli moja kwamba tunataka madawa ya kulevya yawe historia kwenye Mkoa wetu wa Arusha itakuwa hivyo, nimekaa pale Dar es salaam haikuwa rahisi sana mpaka sasa hivi Wauza madawa wakimuona Makonda wanaelewa, wamejaribu mbinu zote za kuroga imeshindika, sumu imeshindikana, wamejaribu mbinu za kuniua imeshindikana”

“Mimi kuna kipindi ilikuwa inakuja drone nyumbani kwangu na Jeshi la Wananchi limenisaidia sana ningeshapotezwa, wana teknolojia ya kukupiga hata na drone lakini kwa mkono wa Mungu ilishindikana, Mimi naishi kwa muujiza, ndio maana unaweza kusema ‘hivi huyu Jamaa ujasiri wake unatokea wapi?’, ni kutoka juu, hapa hamna mzizi wala juju ni kutoka Mbinguni kama Mungu akiamua kuniachilia nipotee ni sekunde tu kwasababu nipo kwenye target zao 24/7”

“Lakini nafurahi kwamba kuna Mtu mmoja nimemuokolea Watoto wake asife kwa dawa za kulevya, niwaombe Polisi hii vita ni ya kujikana, mafanikio ya rushwa ni mbegu ya laana kwenye kizazi chako, Polisi mnisikie, ndio maana Watoto wengi wa Wala rushwa hawako salama”
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad