Yanga Waipiga Mkwara Mkali Simba Kuelekea Aprili 20

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Yanga Waipiga Mkwara Mkali Simba Kuelekea Aprili 20

Joto la Kariakoo Dabi linazidi kupanda ikiwa ni siku nne kwa sasa zinahesabiki kabla ya mchezo huo kuchezwa Uwanja wa Mkapa na kila timu ikiwa kwenye hesabu za kupata pointi tatu.


Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara na vinara wa ligi wamewapiga mkwara watani zao wa jadi kwa kubainisha kuwa wanhitaji pointi tatu za mchezo huo.


Aprili 20 2024 Kariakoo Dabi inatarajiwa kuwa ndani ya uwanja kwa wanaume 22 kusaka pointi tatu uwanjani kwenye mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.


Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa wanaitaka mechi hiyo kwa namna yoyote ili kupata pointi tatu kufikia malengo yao ya kutwaa ubingwa.


“Tunawatazama Simba kwa utofauti hasa kutokana na ubora walionao, nasikia wengi wanasema kwamba timu hiyo haina ubora hilo tunalikataa kwa kuwa ina wachezaji wenye uzoefu.


“Kikubwa ni maandalizi mazuri na kila mchezaji anatambua umuhimu wa mchezo wetu ambao ni mkubwa na Kariakoo Dabi inafuatiliwa na wengi,”..


Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Novemba 5 2023 baada ya dakika90 ubao ulisoma Simba 1-5 Yanga.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad