Ikiwa imepita mda sasa tangu alipogusia swala la kujenga msikiti, ambao utakuwa kumbukumbu yake kwa watakaoutumia, na ikiwa ni
njia moja wapo ya kurudisha katika jamii, Diamond amesema msimamo wake bado uko palepale.

"Sasa hivi mimi nina maeneo yangu, kwasababu ninapokuwa na hela mi nakuwa muoga sana kuwekeza najitahidi sana kununua nunua viwanja au kama hivi vijumba vidogo vidogo vya kuvunja maeneo tofauti tofauti.

Sasa hivi niko plani kwamba niujengee sehem gani, nitengeneze msikiti sehemu ambayo itakua ni nzuri,msikiti ambao hata kesho na kesho kutwa mi nikifa, mababu vizazi na vizazi viwe wanaswali pale kama msikiti ambao aliutengeneza kijana wetu Diamond.Watu wanaswalia, mi naamini itanipa baraka kubwa sana, na soon too naimani mwenyezi Mungu naimani atanisaidia, nitangeneza huo msikiti" amesema Diamond licha ya kuwa na plani ya kujenga mskiti huo.

Iliripotiwa kuwa kwa sasa ameshakamilisha ujenzi wa nyumba ya mama yake mzazi iliyogharimu zaidi ya shilingi za kitanzania milioni 260

 
Top