Maisha ya Polisi: Wengi Wanaishi Chumba Kimoja

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Baadhi ya askari polisi wa chini wanaishi maisha magumu kutokana na kupata kipato kidogo huku wakiishi katika nyumba duni hali inayofanya utendaji wao kushuka

Baada ya shughuli nyingi za kutwa nzima, askari polisi Hashim (siyo jina lake halisi),  anarejea nyumbani kujipumzisha.
Kwa kuwa nyumba anayoishi ipo umbali wa mita 700 kutoka katika  kituo chake cha kazi, Hashim anaamua kutembea kwa miguu.

Anafika nyumbani huku akitokwa jasho mwilini, lakini kabla ya kuingia ndani anawaza mengi, ikiwa ni pamoja na joto lililopo katika nyumba anayoishi na mke wake pamoja na watoto wao wawili.

Nyumba hiyo ni ya chumba kimoja na pia imeezekwa kwa mabati kuanzia juu mpaka chini.
Licha ya kukaribishwa kwa furaha na mkewe, Hashim anaingia ndani kwa unyonge, baada ya kubadili nguo za kazi anakwenda kuoga katika bafu la nje, ambalo hutumiwa na familia zaidi ya 20 za polisi wanaoishi katika nyumba za jeshi hilo (Kota) takriban 25 zilizopo Mtaa wa Mizengo (siyo jina halisi).

Wakati mwingine Hashim hulazimika kwenda katika nyumba ya wageni ili kumaliza faragha na mkewe kwa kuwa anaishi katika chumba kimoja, ana watoto ambao ni wakubwa na siyo jambo la busara kufanya tendo hilo huku wakishuhudia au hata kusikia kwa sababu katika kijumba hicho kidogo wanachoishi, hakuna faragha.

Acha tendo hilo, wakati mwingine hata anapokuwa akitaka kuvaa nguo, watoto ni lazima watoke nje, jambo ambalo linaleta usumbufu mkubwa.

Siyo Hashim pekee, wapo polisi wengi wanaoishi maisha ya aina hii  katika mikoa mbalimbali nchini ambayo yanawafanya washindwe kutekeleza majukumu yao na wengine kuangukia katika vitendo vya kudai rushwa raia ili angalau wazibe mapengo.

Polisi wazungumza
Alipoulizwa kuhusu suala hilo Msemaji wa  Jeshi la Polisi nchini, Advera Senso alisema kwa ufupi, “Unasema wanalalamikia makazi wanayoishi kuwa ni duni…, sasa ingekuwa vyema kama ungetusaidia majina yao ili tuweze kuthibitisha malalamiko hayo.”

Naibu Waziri
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima alisema vitendo vya rushwa kwa askari wa Jeshi la Polisi vinachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza mapato ya taifa hivyo kuifanya Serikali kushindwa kutekeleza wajibu wake.

“Vitendo vya rushwa ni tabia ya askari mwenyewe na kama kuna askari wa juu anamwambia askari wa chini kumpelekea bahasha (rushwa) anatakiwa kutoa taarifa ili waweze kuchukuliwa hatua,” anasema Silima na kuongeza;

“Serikali haiwezi kuboresha mishahara huku wao wenyewe wanapunguza mapato ya taifa kutokana na vitendo vya rushwa, hivyo wanatakiwa kuachana na vitendo hivyo.”
Silima alikiri kuhusu nyumba za askari hao kuwa katika hali duni na kusema Serikali inajitahidi kuboresha makazi ya askari polisi.

“Ni kweli makazi ya askari bado ni tatizo, lakini hivi sasa kama unavyoona tumeshaanza kukabiliana nalo kule Kilwa (jijini Dar es Salaam) tumejenga na mikoani tunaendelea ili nao waishi katika makazi yaliyo bora,” anasema Silima.

Source:Mwananchi
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Msemaji wa jeshi la polisi hana lolote anatetea uozo tu, anataka awajue ili afanyaje? ili hali ukweli anaujua, anachotakiwa nikuchukua changamoto na kuitafutia suluhu....... analeta mtego wa kizamani.

    ReplyDelete

Top Post Ad