Mkurugenzi wa Tanesco Alizwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MKURUGENZI wa zamani wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) aliyefukuzwa kazi  kwa tuhuma za ufisadi, William Mhando, yamemkuta baada ya mtu mmoja aliyejitambulisha kuwa ni mchungaji kumliza magari matano.

Vyanzo vyetu vya habari ndani ya jeshi la polisi vinadai kwamba, Mhando alitinga Kituo cha Polisi  cha Oysterbay na kufungua  kesi na OB/RB/3394 inayohusiana na wizi hivi karibuni.
Taarifa zaidi zinaeleza kwamba,  Mhando alitapeliwa  magari hayo Januari 30, mwaka huu  na mtu aliyejulikana kwa jina la Mchungaji Joseph  anayedaiwa  kuwa anahudumu katika kanisa moja  huko Kigamboni  wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Habari zilizopatikana Kituo cha Polisi Oysterbay zinadai kuwa, magari yaliyokodishwa kwa ajili ya kuwasafirisha  wanafunzi  kwenda kutalii ni aina ya Prado, Nissan Ribert,Rav 4 mbili hadi leo hii hayajaonekana wala mchungaji huyo hajaonekana.
“Polisi wa hapa Oysterbay wanaendelea kufanya uchunguzi  wa kina  kwa sababu magari hayo huenda yameshauzwa na  aliyeyakodisha,” alisema askari mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela alithibitisha kuwepo kwa sakata hilo lakini akasema hajapata taarifa kutoka kwa maofisa wake wanaoshughulikia suala hilo.
William Mhando alipotafutwa kwa njia ya simu ya kiganjani hakuweza kupatikana kwani ilikuwa ikiita bila kupokelewa. 
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad