Ray Atoa la Moyoni Kuhusu Swala la Kukongoroka kwake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Baada ya maneno ya chinichini kumtafuna staa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ kuwa amepungua mwili, ameibuka na kuweka bayana kuwa hakuna kingine kilichosababisha zaidi ya mazoezi.
Hivi karibuni kuliibuka maneno kuwa staa huyo amekonda kupita kiasi ambapo vyombo mbalimbali vya habari viliripoti juu kupungua kwake huko.
Baadhi ya watu wake wa karibu, walianza kuzungumzia sababu ‘chungu mbovu’ huku kila mmoja akisema sababu anazozijua mwenyewe.
Punde baada kurejea Rwanda walipokwenda kuhudhuria tuzo za filamu nchini humo, Ray aliamua kuweka picha zake kwenye mtandao wake zinazomuonesha akifanya mazoezi na kufafanua kuwa amemaliza ubishi kwa wadau wa filamu waliokuwa wakijadili juu kupungua kwake.
“Nikiwa mazoezini… nadhani maswali yatakuwa yamekwisha baaada ya kuwawekea picha hizi…” aliandika Ray mtandaoni.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hana lolote huyo muuza kahawa, c aseme kilichomkondesha au anataka tumsemee,,,?

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwa hyo we una chako cha kusema? C useme 2.. Ray anauza kahawa cku hz? Mbna unaHate 2? Get life

      Delete
  2. Kwakweli kapendeza...sio kipindi kile alivyokua na manyama uzembe...keep it up ray

    ReplyDelete
  3. unene siyo mpango

    ReplyDelete
  4. Afadhal umewafunga midomo yao maana wamezd kufuatilia maisha ya watu yao yanawashinda

    ReplyDelete

Top Post Ad