Wema Sepetu Apata Ajali ya Gari

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



BEAUTIFUL Onyinye, Wema Sepetu amepata ajali mbaya baada ya gari ambalo alikuwa akiliendesha aina ya Audi Q7 kuacha njia na kugonga gari lingine kisha kumgonga mtembea kwa miguu.
Tukio hilo ambalo lilivuta umati wa watu lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita maeneo ya Makumbusho, jijini Dar ambapo ilidaiwa kuwa Wema alikuwa katika mwendo wa kasi na kushindwa kulimudu gari hilo barabarani.

Ajali hiyo ilisababisha foleni na baadhi ya vijana wanaosadikiwa ni vibaka kuanza kumzingira.
Kwa mujibu wa shuhuda aliyeomba hifadhi ya jina, inawezekana alikuwa na mawazo mengi kichwani kwani licha ya kuwa kwenye mwendo wa kasi, hakukuwa na sababu ya wazi iliyosababisha aache barabara.

“Yaani mi nahisi alikuwa na mawazo mengi au alikuwa ‘amepata’ kidogo,” alisema shuhuda huyo aliyedai aliona mchezo mzima.
Baada ya kugonga, ilidaiwa kuwa mwigizaji huyo alishuka kwenye gari na kutaka kumpiga vibao mtembea kwa miguu huyo lakini ghafla watu waliingilia kati na kumzuia huku wakimuonya kuwa akithubutu wangemshushia kichapo.

“Huyu dada vipi? Ajali amesababisha yeye halafu anataka kumpiga mtembea kwa miguu, angejaribu tu tungemvua nguo hapahapa,” alisema shuhuda mmoja aliyekataa kuchorwa jina lake gazetini.

Paparazi wetu alipotonywa na kufika eneo la tukio,  alilishuhudia gari la mwigizaji huyo likiwa limebondeka kwa mbele huku akiliendesha kulipeleka katika gereji iliyokuwa karibu na eneo hilo.

Hata hivyo, Wema alipomuona paparazi akiwa na vitendea kazi vyake  akimfuatilia kwenye gereji hiyo, aliondoa gari lake haraka ambapo umati uliokuwa ukifuatilia kwa makini tukio hilo ulimzomea. Haikufahamika alilipeleka wapi.  
Credits: GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad