Dr Slaa Alikuwa Maarufu Bungeni Bila Lugha ya Kuudhi Wala Matusi, Wabunge Vijana CHADEMA Igeni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Yanayoendelea bungeni kwa sasa yana athari kwa jamii inayoiunga mkono chadema japo wengi hawataki kukubali ukweli huu.

Inawezekana ilikuwa hivyo lakini kwa sasa kitendo cha wabunge wa chadema kutolewa nje kila wakati hakiwajengei tena umaarufu bali kinaanza kuharibu sifa nzuri ya chama.

Umakini wa chadema kwa hili una walakini na mmekubali kuanguka kwenye mtego wa Mwigulu Nchemba na Lusinde kwani wao wakijua kwamba watakapowa-prove na ninyi mka-react mtaendelea kutolewa nje na hili halitaendelea kuwa zuri au kuwapatia umaarufu kama zamani na matokeo yake wananchi watawachoka na kuwaona kama wafanya vurugu.

Mpango huu ulisukwa vizuri kwenye party caucus ya CCM wakimtumia Spika, Naibu wake na hao niliowataja hapo juu, wawachokoze mkiwajibu spika awaadhibu na nyinyi muonekana ndio wakorofi na jamii inayowaamini mwishoni mwa siku itaanza kuaminishwa hivyo.

Nawaomba hata kama spika hataki kutenda haki, daini haki hizo kwa njia za kistaarabu, mna rufaa nyingi ambazo hazijajibiwa, endeleeni kukata hizo rufaa na kuwa bungeni, sitegemei kama makinda hata mlalamike kiasi gani atakuja kuwasikiliza kwa kuwa yuko pale kwa kazi ya kuilinda serikali yake na kuuminya upinzani. Hata mkifanya hayo mnayoyafanya hamtasikilizwa, mfano Mh Lissu alipoambiwa atoke nje angetoka sidhani kama ingetokea damage kubwa kama hii iliyotokea. Kuna wananchi wa majimbo sita ya uchaguzi ambao hawatawakilishwa kwa siku tano, hiki sio kitu kidogo.

Nakumbuka enzi za ubunge wa Dr Slaa, alitajwa na tafiti mbali mbali kama ndiye mbunge kinara zaidi kwa michango na hoja zenye mantiki lakini sijawahi kumsikia akitumia maneno yenye kuudhi kama "this government is impotent'.

Wabunge wa chadema, hasa vijana punguzeni emotions, msiwe driven na maneno ya kuudhi ya akina Mwigulu na Lusinde, hawa wameshajulikana kazi yao ni nini na uzuri wananchi wote wanawajua kama ni wazushi na kila mbinu chafu wanazopanga wananchi wanazijua. Hizo single zao za ukabila sijui Dr Slaa alifanya vikao na viongozi wa dini, sijui ugaidi, haziuzi tena huku mtaani. Kwa hiyo acheni waseme na wakiona hawajibiwi watanyamaza na ndio utakuwa mwisho wao. Nawahakikishia Maneno ya Nchemba na wenzake hayana tena athari kwa chama, kwa kuwa wameshajulikana ni kwa ajili ya kukichafua chama na hakuna ukweli kwa chochote wanachoongea. Waachieni wananchi hao akina Nchemba wataawaadhibu 2015.

Pigeni kazi bila emotions, tuko nyuma yenu, msitafute sababu za kuundiwa kanuni kila siku, hili ndio wanalolitaka akina Makinda. Na hizi kanuni mpya za adhabu ni kwa ajili yenu, hata siku moja hutasikia mbunge wa CCM hata atukane tusi kubwa kama la Serukamba kukemewa wala kutungiwa kanuni. Kanuni iliyowasimamisha haikuwepo na sasa imelazimishwa ili kuwaadhibu ninyi na itaendelea kutumika dhidi yenu. Kuweni makini CCM maji yamewafika shingoni, wanatapatapa wanajaribu kushika hata wimbi la maji wakijua ni gogo la kuwaokoa.

Yangu ni hayo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. NAMNUKULU DR. BENSON BANNA KWA KAULI YAKE KUWA WABUNGE WA CHADEMA ADHABU WALIOPEWA NI NDOGO SANA HATA MIMI NARIDHIA NACHUKULIA MFANO DARASANI MWANAFUNZI AFANYE FUJO NIMWAMBIE TOKA NJE AKATAE NA WENGINE WAMUUNGE MKONO KUWA HATUTOKI SINA UHAKIKA ADHABU YA KUPIGA MAGOTI INATOSHA BUNGENI VIKAO VYOTE VINAGHARAMIWA NA KODI ZA WATANZANIA MASIKINI HOHE HAHE KWA KUWA WABUNGE WANAKULA WANASHIBA NA KUSAZA SINA UHAKIKA WANAFAHAMU WAPO WATANZANIA WASIOKULA UTWASHANGAA WAKATI WAKUOMBA KURA WANAPIGA MAGOTI WANAAMKIA KILA MTU SHIKAMOO SASA HIVI HATA LIFT HAWATOI KWA MTU YE YOTE ILA WAKATI WA UCHAGUZI GARI LINAWEZA KUTUMIKA KUBEBEA WAGONJWA WAKUMBUKWE SASA HIVI TUNAFAHAMU MAANA YA RUSHWA ,ULIAHIDI NINI UMEFANYA NINI USIWE MZURI WA KUNYOSHEA WENZAKO MKONOKIDOLE KIMOJA WAKATI VIDOLE VINNE VIKIELEKEA KWAKO FAINALI UCHAGUZI 2015

    ReplyDelete

Top Post Ad