Linex Aongelea kuhusu Mama yake Kukasirika yeye Kumvisha Binti wa Kizungu Pete

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Stori:Chande Abdallah na Issakwisa
Wiki iliyopita kwenye Funguka na Risasi tulikuwa naye Mh. Nyambari Nyangwine akifungukia kuhusiana na skendo yake ya kukimbia kambi ya mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Wiki hii tunaye msanii wa Bongo Fleva, Sunday Mangu ‘Linex’ akifungukia kuhusu mapenzi yake na mchumba wake wa Kizungu aliyemvisha pete siku kadhaa zilizopita, Suvi Rikka.
Funguka: Mambo vipi Linex?

Linex: Shwari tu niaje?
Funguka: Poa, tuna maswali kadhaa kuhusu uamuzi wako wa kumvisha pete ya uchumba msichana wa Kizungu, vipi marafiki na ndugu zako wanazungumziaje jambo hilo?
Linex: Hakuna mtu aliyezungumzia vibaya suala hilo wala kupinga kitendo nilichokifanya, isipokuwa mama yangu tu ndiye alikasirika kidogo kwa sababu sikumtaarifu mapema.
Funguka: Ndugu wa mchumba wako wanakuchukuliaje, hawakubagui kutokana na rangi na utaifa wako?
Linex: Hapana hawanibagui hata kidogo, wao hawapo hivyo, Wazungu siyo watu wakufuatiliana na kuwekeana mipaka kwa mambo kama hayo.
Funguka: Nini ambacho unakiona katika uhusiano wenu ambacho pengine hukukiona katika awali kwa wasichana wengine wa Kibongo?
Linex: Mapenzi ni mapenzi tu, hakuna jipya sana, zaidi ya uwazi na ukweli kwa kila jambo, hajawahi kunidanganya hata siku moja.
Funguka: Lakini Linex kwa nini yeye na siyo madada zetu wa Kibantu ambao pengine walikuwa wakitamani sana kuvishwa pete na wewe siku moja?
Linex: Sina maana labda kuwa na mchumba wa Kizungu sijawaona wa Kibantu, ila imetokea tu, hata mimi mwenyewe sijui ilikuwaje! Naamini hakuna mwanamke mzuri kama wa Kibantu ila ndiyo hivyo tena imeshatokea, si unajua tena kupenda!
Funguka: Unaamini kama Wazungu wengi wanavutiwa kimapenzi na wanaume wenye dredi?
Linex: Hapana, siamini hata kidogo na wala sijawahi kuwaza hivyo kabisa.
Funguka: Poa kaka siku njema tutakucheki.
Linex: Haina noma wakubwa, karibuni.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mwacheni mzazi apewe English course! Sa nyingne c wabongo twapenda mauzo na c Mapenzi

    ReplyDelete
  2. Do go hajui alipo,chokolaa kama yy future ya kuungaunga anadhani mzungu ni zali la mentali

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeona eeh!lazima achemke dogo anafikiri atamlisha huyo mzungu dagaa daily

      Delete

Top Post Ad