Diamond Platnumz "Jokate Nisamehe"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MKALI wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, ameibuka na kuelezea kuhusu uhusiano wake na mpenzi wake zilipendwa, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ ambaye ni mwigizaji na modo moto wa kuotea mbali Tanzania.
Akizungumza kwa uhakika kabisa, Diamond alisema inampasa amuombe radhi Jokate kwa sababu katika uhusiano wao, Jokate hakuwahi kumkosea ila yeye ndiye tatizo na chanzo cha kuachana kwao.
Diamond alisema hayo kwenye mahojiano na Mtangazaji Zamaradi Mketema katika Runinga ya Clouds kwenye Kipindi cha Take One, kilichorushwa juzi Jumanne usiku kituoni hapo.

DIAMOND ANAFAFANUA
“Inanipasa nimuombe radhi Jokate. Ni kweli nilimtenda vibaya wakati wa mapenzi yetu. Hakukosea sana maana hakuwahi kufanya jambo lolote kinyume. Sijui niseme nini lakini nataka kueleza wazi kuwa mimi ndiyo sababu ya kuachana kwetu na ilitokea tu.

“Naamini hilo jambo lilimuuma sana, maana nakumbuka wakati ule, baada ya mimi kurudi kwa Wema (Sepetu), watu walimwandama sana kwa maneno na alionekana msaliti lakini ukweli ni kwamba nilimpenda sana lakini ndiyo hivyo, siwezi kufafanua zaidi.
“Kutoka moyoni mwangu, namuomba msamaha Jokate, kama hatanisamehe nitaendelea kumuomba mpaka naingia kaburini. Sina raha kabisa kutokana na jambo hilo. Lazima niwe mkweli.”

JACQUELINE WOLPER
Diamond alikwenda mbali zaidi na kuwazungumzia baadhi ya wasichana aliowahi kutoka nao kimapenzi akiwemo mwigizaji Jacqueline  Wolper ambaye alisema ni mwanamke aliyempenda sana, ndiyo maana alimtungia wimbo wa Mawazo.

PENNY SASA
Kwa upande wa mpenzi aliye naye sasa, Mtangazaji wa Runinga ya DTV, Penieli Mungilwa ‘Penny’ alisema ni mwanamke mtulivu na sahihi kwake kwa sababu anatambua majukumu yake kwake, pia anamheshimu.
“Huyu kwa kweli ana karibu sifa zote alizonazo Wema ila uzuri wa Penny ananiheshimu sana. Hafanyi mambo yake hadharani. Unajua wakati nikiwa na Wema hata kama akifanya mambo yake siku mbili au tatu baadaye nayaona kwenye magazeti, tofauti na Penny ambaye kwangu mimi naona ananiheshimu, hata kama anafanya mambo yake ni kwa siri.”

Source:GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Dah tumechoka story za huyu Dimond..... Zooote nikihusu wanawake tu! Jamani hatuzihitaji mbona mnatulazimisha??? Akiwa najipya ok tujulisheni..... Alwayz Wema,Joket,Peny Jaklin TUMECHOKAAAAAAAA......

    ReplyDelete
  2. wacha kuendekeza ngono utazikwa siku si zako!

    ReplyDelete
  3. wacha kuendekeza ngono utazikwa siku si zako!

    ReplyDelete
  4. ala, Kumbe hata Wolper naye alishaliwa na dogo huyo? Nilidhani ni tetesi tu kumbe ni kweli hadi akamtungia wimbo wa mawazo.

    ReplyDelete
  5. badala ya kumwomba wema msamaa unamwomba joketo hovyo

    ReplyDelete
  6. diamond mwenyew wala c handsome mbona kuna wasanii ma HB ila hawana scandal za kijinga mi binafs wala cmpend na wala hakustahil kua na wema wala joket

    ReplyDelete
  7. Hajielewi Nassib in short unajiaibisha na kujiandalia mwisho mmbaya.mnasema vijana muwe makini wanawake kama nguo chagua mmoja uoe.na wewe ni muislamu mwenyezimungu anakuona


    ReplyDelete
  8. Anaona maujiko kutuwekea idadi ya wanawake aliotembea nao wote hao ni mbululu tu.

    ReplyDelete
  9. Ivi hao wanawake wote atawaoa? Au kuwachezea tu, then wanawake wenyewe wanaona sifa sana kuchezewa!

    ReplyDelete
  10. Duh..... dogo 2 much,but angalia future ucjefulia kama kina mr nyc

    ReplyDelete
  11. We kjana hv una ndugu kwel,ka unao wanajckiaje kuckia mapenz kla cku bwana

    ReplyDelete

Top Post Ad