Lady Jay Dee "Siku Nikifa Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi
Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.
Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.
Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.
Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.

Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.
Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria.Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.
Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.
Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao.
Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.
Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame. Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.
Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai. Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.
Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.
Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge.
Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.
Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia..
Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..
Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.
Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani?? Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??
Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.
Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.
Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma?? Roho gani hiyo??
Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu
JIDE
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

32 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mmmmmmmmmmmhhh makubwa haya

    ReplyDelete
  2. big up kaza buti dada kwani wafitini hawakosi hapa duniani. Na pia kunawatu wanataka wawe mbele pekee yao tu. songa mbele usife moyo!

    ReplyDelete
  3. Life is the journey with the lot of changes and uncertainties. Hawa ndio wanaitwa binadamu ni wanang'ata kuliko hata simba wa porini.

    ReplyDelete
  4. huyo Ruge ndo nani?kaza mwendo dada sisi mashabiki ndio tunajua kila kitu.nashukuru kwa kuwa umekomboka kifikra.

    ReplyDelete
  5. Dada jide, usiogope maneno, we utabaki kuwa juu tu. Zidi kumwomba mungu

    ReplyDelete
  6. amefunguka vya kutoshaa....kazi kwao hao jamaa na wananichefua mbaya.
    Komaaaa mama uckwamee

    ReplyDelete
  7. Kusaga analamba matako ya ruge tokea A city uwakiwaaa mawinguuu club

    ReplyDelete
  8. Yes, HUyu Ndio Komando Bwana,Sema dada,Wewe ni mwanamuziki Kiongozi kutoka Tanzania. Wanastaili wakubembeleze sio wwe uwabembeleze.Go Jide Go Jide Go Jide.watakufa watakuacha unadunda kama kawa

    ReplyDelete
  9. U made i dada, komando jide

    ReplyDelete
    Replies
    1. hii kali ya mwaka!!! matapel wapo weng wataka kula bila jasho!!

      Delete
  10. Jide na hiyo guarantee,usituyumbishe NA kutuaminisha hicho,kwani ukipatanishwa NA kupigiwa nyimbo zako utatulia.Mr 2 amepatanishwa bifu ilikua Kali sembuse ww.pi a nalaumu huyo mwanaume kama binti ulienae,kalelewa NA clouds y asifanye the needful kukupoza.ngo'orong'ondo wakubwa nyie

    ReplyDelete
  11. dada hongera kwa kufanya yako
    yaan cjawah kuona umefanya collabo na msanii wa hip hop halaf nyimbo ikawa mbaya we ni mkali of all time

    ReplyDelete
  12. Jide Mtangulize Mungu mbele hao Ruge na Kahaba wake Mutahaba wazushi tu labda walikua wanakutaka uwape uroda maana ndio tabia za vibosile wa kibongo,Weee Komando Anakonda nakuaminia utasimama kwa miguu yako na kudra ya Mungu hongera kwa kuwa muwazi.

    ReplyDelete
  13. Duuuh jide umesema ukweli,ila radio haipo moja zipo nyingi tu,yan mngeungana wanamuziki woooteee yan wooote msiwabembeleze hao wajinga ndo wanafanya mziki usikue nchini,maana nyie msipokua na pesa unafikiri tasnia yenu itakua?sikia tumieni startv,dtv,EATv,hawa hawana noma,radio one,yan hawana noma halafu ndo zinawatazamaji wengiiii,ila kwa sababu wanamziki wa bongo na watanzania kwa ujumla ni waoga hawawezi fanya kitu chochote,wao ni ndio boss ndio boss,ila pia wanasifika kwa uzurumishi hahahahahahaha

    ReplyDelete
  14. what the fuck happening in this industry, wamepigiwakelele lakini hawabadiliki, aibu iko juu yao

    ReplyDelete
  15. Umeliona hilo baada ya kukufanyia fitna ukashindwa kufungua kituo chako cha radio. Tatzo komando unaanzisha ugomvi wa mawe wakati nyumba yako ya vioo. Jipange upya sasa. Tafta timu ya washauri wasomi wa fani mbali mbali wakuelekeze nini cha kufanya. Njia unayotumia kushindana nayo wewe ndo utashindwa.

    ReplyDelete
  16. Komaa Msubhati we ni komando wa kweli

    ReplyDelete
  17. Mtegemee Mungu dada Jide, hata siku moja usiwategemee binadamu, hao kina Ruge ni binadamu tu wasikubabaishe, Hakika Mungu atakusimamia.

    ReplyDelete
  18. I AVE EVER SEEN AN IRON LADY AS YOU JIDE, SO FAR YOU HAVE BEEN THE ONLY COMMANDO LADY IN BONGO FLEVA EVEN THEIR "CAVINGS" CANT GET YOUR LEVELS. LET THEM DO WAT THEY WANT BUT THEY CANT TAKE YOU DOWN. MORE THAN 13 YEARS IN THE GAME AND YOU STILL ROCK HATTERS FEEL SHY. RUGE AND KUSAGA TO HELL.............

    ReplyDelete
  19. SIO POA WANAVYOFANYA KOMAA DADA WE NI KOMANDO MKO WACHACHE KAMA NYINYI UELEWA MKUBWA PEOPLE THEY NEED TO GROW THIS WAY your so real sis.

    ReplyDelete
  20. Hongera kwa kuyamwaga hadharani. Waaibike na kufedheheka wote wanaodidimiza jitihada za wengine katika maisha. HiloooooooooooooooooooooooooooAcheni mabo yenu Kusaga. Nilikuwa nakusikia kama mtu wa maana kumbe.....utajaza mwenyewe!!!!!!!!!!!Ichube

    ReplyDelete
  21. pole kila penye mafanikio hapakosi fitina
    so don mind

    ReplyDelete
  22. Nataman ningesikia upande wa pili.ila dada yangu lainisha moyo wako.ukitaka mafanikio zaid yabid kumwombea adui yako ili aje aone mafanikio yako zaid.

    ReplyDelete
  23. Pole yote ni mapito ya dunian,sali sana ili wakupishe songa mbele

    ReplyDelete
  24. JIDE WEWE NI JEMBE DADA NAJUA UKITAFUTA WASANII WAKONGWE KAMA PR JAY MKAJIPANGA MTATISHA SANA ACHANA NA HAYO MAGUBE GUBE

    ReplyDelete
  25. Ww Mkali dada jide miaka Mia nane hamcin unawakimbiza hao ni Mende tu Kama Mende wengine so wackutishe kaza buti wazidi kuona mafamikio yako

    ReplyDelete
  26. Poleeee dada jide hayo ni majungu tu ss mashabiki wako tunakukubali ile mbaya yaani weweee ni nomaaaaaaaaa.

    ReplyDelete
  27. Uko juu acha waongee

    ReplyDelete
  28. kwani kuna mtu mwenye akili timamu anaesikiliza tena CLOUDS FM? dada Jide achana na hao mambulula akili zao zimeganda wanaona kwamba wao ndo wapo right all the time, clouds fm kitu gani wasipopiga nyimbo zako zitapigwa kwingine kama Magic fm, East Africa fm, kiss,rfa, times fm na nyingine kibao pamoja na radio za kanda au na hizi pia ni za ruge?????????????

    ReplyDelete
  29. Tunahitaji wasanii jasiri kama hawa. huu ni mfano kwa wasanii wengine wanaonyonywa na hawa fisi maji. MSANII amka sasa. safi sana DADA JIDE

    ReplyDelete
  30. I love u jide,mamaaa sam fud

    ReplyDelete

Top Post Ad