List ya Wasanii Maarufu Bongo Walio Badili Dini kwa Ajili ya kubembeleza Ndoa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

ULIMWENGU wa mastaa duniani kote huwa unatawaliwa na vituko, vimbwanga na kubwa zaidi ni mapenzi kwani ni sehemu ya mambo yenye mguso wa aina yake katika jamii.
Leo katika ukurasa huu tunakuletea mastaa wa Kibongo ambao wamebadili dini kwa ajili ya ndoa au uhusiano wa kimapenzi wakijiandaa kuelekea kwenye ndoa.

Wapo waliofanikiwa kuingia kwenye ndoa lakini wengine wameambulia kuachana na kubaki njia panda kuhusu suala la dini, yaani wabaki upande gani.

JACQUELINE PENTZEL
Ni msanii wa filamu za nyumbani na Bongo Fleva. Mwaka huu mwanadada huyo alibadili dini akasilimu ndipo akafunga ndoa na jamaa aitwaye Gadna Dibibi.
Kwenye mahojiano Jack alikiri kuwa alilazimika kubadili dini kwa kuwa alimpenda mwanaume huyo hivyo akaamua kufuata dini yake.

JACQUELINE WOLPER
Wolper ni staa wa filamu za nyumbani na video za Bongo Fleva. Alisilimu baada ya aliyekuwa mchumba’ke, Abdallah Mtoro ‘Dallas’ ili afunge naye ndoa.
Baada ya Wolper kusilimu alipewa jina la Ilham lakini siku chache uhusiano wao uliota mbawa na mipango ya ndoa nayo ikayeyuka.
Wolper aliwahi kukiri kuwa baada ya kutokea hali hiyo hawezi kurudi tena nyuma kwenye Ukristo kwa sababu atakuwa anamchezea Mungu hivyo hajielewi yupo sehemu gani kwa sasa.

ROSE NDAUKA
Ni bidada kutoka kiwanda cha filamu Bongo. Rose alibadili dini baada ya kupata mchumba aliyekuwa memba wa kundi la muziki la TGN la Tanga, Malick Bandawe.
Hadi sasa ni wachumba lakini ndoa wamekuwa wakisema leo, kesho hali inayowachanganya baadhi ya watu kwani ni muda mrefu tangu walipoanza kusema hivyo.

FLORA MVUNGI
Ni msanii wa filamu na Bongo Fleva ambaye alibadili dini baada ya kumpata mchumba Muislam ambaye ni mwanamuziki wa Bongo Fleva, Hamis Ramadhan Baba ‘H. Baba’.
Flora kwa sasa anajulikana kwa jina la Hadija ambapo wamekaa kwenye uchumba muda mrefu kabla ya kufunga ndoa Juni 8, mwaka huu huku akiwa mjamzito.

AUNT EZEKIEL
Mwanadada huyo kutoka kiwanda cha filamu ameolewa baada ya kusilimu na kuolewa na Sunday Demonte huku wakiishi sehemu tofauti, Aunt yupo Dar na mumewe yupo Dubai.

OTILIA BONIFACE
Ni mnenguaji wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo Staili’. Alisilimu baada ya kupata mchumba anayedaiwa kuwa ni mume wa mtu, anayetajwa kwa jina la Ali K. hadi sasa hawajafunga ndoa lakini wanaishi pamoja kama mke na mume.

MICHAEL SANGU ‘MIKE’
Ni mwigizaji wa kitambo. Aliwahi kusilimu ili afunge ndoa na mwigizaji mwenzake, Kulthum Mpalu ‘Ummy’ ambaye walifanikiwa kupata mtoto mmoja kabla ya ndoa hiyo kuvunjika.
Baada ya Mike kuona ndoa imevunjika aliamua kurudi kwenye dini yake ya Kikristo na kumuoa msanii mwenzake, Salome Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ ambaye ndoa yao inaendelea vizuri.

JIMMY MAFUFU
Ni msanii wa filamu za Kibongo. Hivi karibuni alisilimu ndipo akafunga ndoa na mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Salma.

Source: GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad