SIRI KUBWA YATANDA KUHUSU KUNYONGWA KWA WATANZANAIA WAWILI WALIONASWA NA MADAWA YA KULEVYA HUKO NCHINI MISRI..!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Sharifa Mahmud (27) akiwa mbele ya dawa za kulevya anazodaiwa kukamatwa nazo nchini Misri
SAKATA la Watanzania wawili waliokamtwa na dawa za kulevya nchini Misri imezidi kuwa na usiri mkubwa, baada ya ndugu zao kushindwa kupata ukweli juu ya uhai wao na tuhuma zinazo wakabiri.
Akizungumza na Mwanadishi wetu  jijini Dar es Salaam ndugu wa karibu na watuhumiwa hao ambao ni mtu na binamu yake, alisema kwamba serikali ya Misri imeendelea kuficha ukweli wa suala la ngudu zake kukamatwa na dawa za kulevya.
"Bado tunahangaika kupata taarifa kamili juu ya maisha ya ndugu zangu, tumeweza kuwasiliana na ubalozi wa Misri nchini Tanzania wakasema kwamba hawana taarifa sahihi juu ya suala hilo, tukawasiliana na Serikali ya Tanzania kupitia ubalozi wake nchini Misri, lakini taarifa tuliyopata ikatupa utata zaidi"alisema ndugu wa watuhumiwa hao kwa masharti ya kutotajwa jina lake mtandaoni.
Alisema kwamba "Ubalozi wa Tanzania nchini Misri uliweza kuwasiliana na Mamlaka zinazohusiana na kitengo cha dawa za kulevya na kukutana na watuhumiwa hao, ambapo walituwezesha kuzungumza nao kabla hawajapandshwa Mahakamani lakini baada ya hapo upatikani wa taarifa zao zimekuwa za siri sana" alisema mtoa taarifa huyo na kuongeza:. Mpaka hivi sasa hatuelewi kinachoendelea,mawasilaino yamekuwa magumu ingawa hatujakata tamaa ya kuwasiliana na ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Misri" 
Watuhumiwa hao wenye undugu wa mtoto wa Mjomba na Shangazi wakazi wa Magomeni na Ilala jijini Dar es Salaam ni Mbarak Abdallah (28) na Sharifa Mahmud (27),  walikamatwa Mei 16 mwaka huu nchini humo  wakitoka Jijini Dar es Salaa kupitia Nairobi nchini Kenya, wakiwa na dawa ya kulevya aina Heroine kilo saba. Baada ya kukamatwa Mei 18 mwaka huu Ubalozi wa Tanzania nchini Misri uliitwa kwenda kuwatambua na baada ya kubainika kwamba ni watanzania walirudishwa rumande baada ya kuzungumza na ndugu zao nchini Tanzania. Mei 26 walipelekwa Mahakamani kwa mara ya kwanza na kurudishwa rumande.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tatizo vijana mnataka utajiri wa haraka ona sasa.

    ReplyDelete
  2. Tatizo vijana mnataka utajiri wa haraka ona sasa.

    ReplyDelete
  3. wapewe haki yao i mean adhabu

    ReplyDelete
  4. Nyie kweli udaku mnaandika unafiki tu ndugu zake gani mloongea nao huyo mwanamke ana pasport ya oman ubalozi watanzania unahusika vipi na yeye ni raiya wa OMAN. Serekali ya oman imemchukua kwa kubadilishana wafungwa na amehukumiwa miaka 18 jela. Km hamjui bora mnyamaze msiropoke, shame on you

    ReplyDelete
  5. Madawa ya kulevya ni sumu kwa jamii,wakinyongwa ni sawa tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad