DIAMOND AFUTURU NA KIMADA!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

HIVI karibuni mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ amenaswa akifuturu na hawara yake, Penniel Mungilwa ‘Penny’, kitendo ambacho kimewashangaza wengi na baadhi kufikia hatua ya kumponda kuwa anakwenda kinyume na Uislam.
Tukio hilo lilijiri nyumbani kwa Diamond maeneo ya Sinza- Mori jijini Dar ambapo mbali na mastaa hao, pia walikuwepo waumini wengine wa dini hiyo walioalikwa katika chakula hicho kitakatifu.

Waumini wamponda
Wakizungumza na gazeti hili mara baada ya kumuona Penny ambaye ni demu wa Diamond akiwa eneo hilo, baadhi ya waumini walisema walishangazwa na uwepo wake kwani sheria ya dini ya Kiislam hairuhusu kuwa karibu na kimada hasa katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Walisema, Diamond hatakiwi kuwa karibu na Penny si kwa kipindi hiki tu bali hata baada, mpaka pale ambapo atatoa mahari na kuozeshwa kwa kufuata misingi ya dini ya Kiislam.
“Huyu kijana kafanya jambo zuri la kuwafuturisha wenzake ila amekosea kumualika yule mwanamke wake, yule kwake ni kimada na kwa sheria za dini yetu huruhusiwi kabisa kumkaribia, sasa ona wanafuturu pamoja na wanashikanashikana, ile siyo sawa,” alisema muumini mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Swaleh alisema: “Diamond anatakiwa aambiwe kuwa anafanya makosa sana kuwa karibu na yule Penny.
“Kihalali kwanza anatakiwa amsilimishe kisha amlipie mahari ndipo amuoe lakini kinyume na hapo atakuwa anaishi na hawara na kuwa naye karibu ni kujichumia dhambi anazoweza kuziepuka.”

Mashehe nao wacharuka
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, baadhi ya mashehe wenye heshima kubwa Tanzania nao walionesha kukerwa na kitendo alichokifanya Diamond na kusema kinakiuka maadili ya dini yao.
Walisema, mwanamke ambaye hajaolewa anayeishi au kuwa karibu na mwanaume na wakati mwingine kuzini, huyo ni kimada na hana nafasi kwenye Uislam.

Shehe Khamisi Mataka
Huyu ni Katibu Mkuu wa Taasisi ya Mashehe na Wanazuoni Tanzania anasema: “Lengo la swaumu ni kumfanya mtu kuwa Mchamungu na Mchamungu ni yule anayefanya yale aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu na kuacha aliyokatazwa.
“Katika Uislam kuwa na hawara inakatazwa, si kwa kipindi hiki tu cha Mwezi Mtukufu bali hata baada. Kwa hiyo kufuturu na hawara ni kinyume na Uislam na unapata dhambi.”

Maalim Hassan Yahya
Ni Mnajimu maarufu nchini. Yeye anasema kuwa, hawara hakubaliki kidini hivyo hatakiwi kupika futari wala kuwa naye karibu kwa namna yoyote, kufanya hivyo ni kwenda kinyume na taratibu za funga na maadili ya Uislam.

Shekh Alhad Musa Salum
Huyu ni Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kuhusiana na hili la Diamond la kufuturu na Penny anasema kuwa, uhawara hauruhusiwi katika Uislam na wanaoendekeza hilo waache mara moja ili waweze kupata radhi za Mwenyezi Mungu.
Shehe Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaaban Simba hivi karibuni aliwasihi Waislam kutimiza nguzo hiyo muhimu ya Uislam na kuwataka wahakikishe wanafuata sheria na taratibu zilizowekwa ili waweze kufikia lengo la kufunga

Source:GLP
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kaka abdul vipi kuweni mkiuliza kabla yaku tenda jambo nindi uungwana

    ReplyDelete
  2. Analeta u supastaa kwenye dini,sio mfano mzuri hata kidogo.

    ReplyDelete
  3. Hy kali.mm mwenyew nk mbal na mume wng mtarajiwa ht cm cpgiw mpk saa moja.ajfunzeee

    ReplyDelete
  4. Allah ni yule yule na sheria zake ni zile zile hazibadiliki kamwe..ukiwa na tabia za kumuasi miez mingine kwa nini ushindwe ramadhan.mwambieni AAACHE UTOTO HUYO DOGO LEO YUKO KULEE KESHO YUKO HAPA. Kul naefsi dhaalikal mauti

    ReplyDelete
  5. Hawa mashekhe wanafiki, kama ndio DIamond kakosea kwanini wao kama masheikhe wasimuite pembeni wakamuelimisha nakumwambia?. Lazima waniike ktk internent that Diamond kamualika girlfriend wake?. Very pathetic.

    ReplyDelete

Top Post Ad