IRENE UWOYA NA LUCY KOMBA WASHIKANA UGONI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

NYOTA wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya ‘Mama Krrish’ ametoa kali ya mwaka baada ya kudai kwamba amemshika ugoni msanii mwenzake, Lucy Komba mara baada ya kuziona picha za msanii huyo akiwa na mumewe, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ wakiigiza filamu.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kutokea nchini Swaziland, Uwoya amepinga vikali utetezi unaosemwa kwamba Lucy na Kataut walikuwa wakishuti filamu na anaamini kuwa msanii huyo ameamua kumzunguka na kutaka kuibomoa ndoa yake.

“Lazima kuna kitu kinaendelea kwani katika dunia hii sijawahi kuona filamu inayochezwa na watu wawili tu mwanzo mpaka mwisho, ninachotaka kusema  ni kwamba Lucy ana mpango wa kuiharibu ndoa yangu,” alisema Uwoya kwa hasira.

Uwoya amehoji usiri wa filamu hiyo na kila alipokuwa akimpigia simu mumewe alikuwa akimjibu kwamba yuko Rwanda kumbe alikuwa Bongo akiigiza filamu na Lucy.
 

“Kwanza Lucy ashukuru niko mbali, laiti ningekuwa karibu angenieleza vizuri kwa sababu hata yeye angeweza kunipigia simu na kunifahamisha ushiriki wa mume wangu kwenye filamu hiyo kwa kuwa namba zangu anazo, ilikuwaje hakufanya hivyo?” alihoji.

Kuonesha kwamba amechukizwa na kitendo hicho, Uwoya alisema kwamba akitua Bongo atamtafuta Lucy ili aweze kumshughulikia vizuri na ikiwezekana amuoneshe hiyo filamu waliyoigiza watu wawili tu.

“Nitatua Bongo siku si nyingi na cha kwanza ni kumtafuta Lucy, anieleze vizuri kuhusu filamu hiyo waliyocheza na mume wangu,” alisema Uwoya.

Filamu hiyo ambayo imekuwa maumivu makubwa kwa Uwoya, imechezwa na Lucy na Ndikumana tu mwanzo hadi mwisho na imepewa jina la Kwa Nini Nisikuoe. 
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Innocent safari24 July 2013 at 18:27

    We ulisema chanin,mwenzako akasema nitakipata lini.

    ReplyDelete
  2. Malaya mtaka vyote mme utakua nae ww. Ushamtesa vya kutosha mkaka wa watu. Mwache aishi maisha yake.unawivu uku wewe unafumaniwa kila siku. Kweli nimeamini Malaya wengi ndo wanawivu

    ReplyDelete
  3. Wewe ukimuona wa nini wenzio wanajiuliza watampata lini, namshangaa huyo Irene kujifanya kuhoji wakati mwanamme kamshindwa mwenyewe. Lucy mama ikiwezekana kama ni kweli mnadate chukua chombo kimoja hamna kulegeza uzi. Mwanaume anahitaji kuenziwa bibi yamekushinda waachie wenye meno watafune.

    ReplyDelete

Top Post Ad