MADEE AKAGULIWA LISAA LIMOJA UWANJA WA NDEGE SOUTH AFRICA KWA HOFU KUWA ANA MADAWA YA KULEVYA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kwenye Exclusive interview na millardayo.com Madee amehadithia kila kitu kilichomtokea wakati anaingia tu Afrika Kusini siku kadhaa zilizopita ambapo hii imetokea kutokana na ukubwa wa habari, uzito wa tukio la wale Watanzania wawili wasichana waliokamatwa kwenye kiwanja cha ndege Johannesburg wakiwa na dawa za kulevya wakitokea Tanzania.
Madee anakwambia alipotua kwenye kiwanja cha ndege, kawaida huwa kuna utaratibu wa kuchekiwa hati ya kusafiria na ukaguzi mwingine ambao hufanywa na mitambo maalum kwa kila abiria anaeingia Afrika kusini, ni ukaguzi ambao unafanywa Airport kabla ya abiria kuruhusiwa kuingia kwenye nchi yenyewe.
Kilichomfanya Madee kusachiwa na kuhojiwa karibu dakika 60 ni pale tu aliposema anatokea Tanzania, kuna wazungu wawili wenye sare tofauti za kipolisi wakaanza kumsachi mpaka kufikia kumwambia avue t shirt yake, alivua t shirt na kubakiwa na nguo nyepesi ya ndani wakati huo abiria wenzake aliokwenda nao walikua wameruhusiwa.
Kati ya abiria wote waliokuja pamoja kwenye ndege, Madee na Mzimbabwe mmoja ndio walikaguliwa sana ila huyo mwingine alikaguliwa kidogo tu kama dakika 10 na wala hakuambiwa avue nguo.
Sehemu yenyewe Madee aliyoambiwa avue nguo sio kwenye chumba maalum, ni palepale kwenye foleni wanaposimama watu ila kwa pembeni kidogo, ni sehemu ambayo imezibwa na kioo kinacholingana na usawa wa tumbo kushuka chini…. Madee anakwambia jamaa walinong’onezana sana wakati wanamkagua.
Hata hivyo baada ya Askari hao kumuweka sana msanii huyu wa bongofleva kutoka kundi la TipTop Connection walimuomba radhi baada ya kumaliza ukaguzi wao ambao pia ulihusika kulivuruga sana begi lake.
Unataka kupata stori kamili? sikiliza AMPLIFAYA ya Clouds FM leo saa moja usiku, pia kwa Breaking News, habari yoyote ambayo ni habari, vituko, vichekesho, videos na music na mengine… jiunge kuwa mwanachama wa millardayo.com kupitia facebook https://www.facebook.com/millardayo au twitter https://twitter.com/millardayo pia instagram.com/millardayo ili uwe wa kwanza kutupiwa link kila tukio linapoandikwa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ADMIN HAPA KUNA KITU NATAKA NIKUREKEBISHE BWANA. HAMNA KITU KINAITWA LISAA LIMOJA KISWAHILI HALISI NI SAA MOJA... NAFIKIRI UMENIELEWA.

    ReplyDelete
  2. ADMIN HAPA KUNA KITU NATAKA NIKUREKEBISHE BWANA. HAMNA KITU KINAITWA LISAA LIMOJA KISWAHILI HALISI NI SAA MOJA... NAFIKIRI UMENIELEWA.

    ReplyDelete
  3. Mdau hapo juuu kuna kitu kinaitwa aqcent!!!matamshi yako na mimi na yule Never be the same,as long as umeelewa nini kinachozungumziwa toa comments sio kusaisha watu wameandika nini,Pole Madee kwa kukaguliwa muda wote huo,wako kazini hao usijali mradi umepita salama!!?

    ReplyDelete

Top Post Ad