MWANAMUZIKI LINAH SANGA AKANA VIKALI KUBAKWA-MSIKILIZE HAPA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mrembo na mwanamuziki wa kike nchini, Linah Sanga amezikanusha ripoti zilizosambazwa leo kuwa amebakwa na rapper Kimbunga na kudai kuwa ameshangazwa mno na taarifa hizo.
Taarifa hizo zimeanza kusambazwa leo mchana baada ya akaunti ya Facebook inayoonekana kuwa ya rapper Kalapina yenye jina ‘KalApina Kikosi Cha Mizinga’ kuandika:

“Mtoto kimbunga amechamba ana leta usela mavi mambo ya kizamani hivi yupo chini ya ulinzi osterbay police kwa kosa la kumbaka msanii lina.”

Bongo5 imezungumza na Linah ambaye amesema amepigiwa simu na watu wengi wa karibu kumuuliza suala hilo wakiwemo, Barnaba, Ditto, Amini na mtangazaji wa Clouds FM, Soudy Brown.

Amesema Soudy alimwambia kuwa ameziona taarifa hizo kwenye Facebook kwenye akaunti ya Kalapina.

“Sasa nikasema Kalapina ameandika hivi, kwasababu sijaingia mwenyewe kuangalia chochote. Sikutaka kujipa stress kwasababu kuna kazi nafanya nisije nikaharibu kazi kwahiyo nikaona vitu vingine kama hivi ni vya kupotezea tu lakini sio vizuri kabisa yaani. Kiukweli sijapenda, yaani bora mtu anizushie kitu kingine chochote lakini si suala kama hilo hapo, si suala zuri,” amesema Linah.

Amesema jana usiku alitoka na mpenzi wake kwenda kwenye sinema na wakarejea nyumbani salama.

“Sasa sielewi huko kubakwa nimebakwa saa ngapi na nilikuwa na boyfriend wangu labda yeye ndio kanibaka! Maana mtu wanayeniambia amenibaka Kimbunga, huyo Kimbunga hata simjui, namskia tu.Nashindwa kuelewa, kwanini mtu azushe kitu kama hicho yaani ndo nataka kujua source ni nini. Niko fine yaani, kwasababu naelewa ‘it’s not true, lakini nafikiria huyo mtu mpaka kaamua kunifanyia kitu kama hicho, nimemkosea nini au kuna kitu gani, yaani hicho ndio kinaniumiza kichwa.”

MSIKILIZE HAPA:

Source:Bongo 5
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. sawa kwanza mtu mzima habakwi anataka mwenyewe tu.... Lina usiwaze bongo kuna kuna watu wanakula na kunya na kulala kupitia uzushi so "No Worries"

    ReplyDelete
  2. Yes mtu mzima habakwi huwa amekubali mwenyewe

    ReplyDelete
  3. NINAVYO JUA MIMI NI YEYE KALAPINA ALIWAHI KUBAKWA WAKATI AKIWA MDOGO,LABDA HII KITU IMEMCHANGA KIAKILI,KAMAKUNAMTU ANAWEZA KUMSAIDIA AMSADIE MAPEMA KABLA HAJARUDIA UJINGA KAMA HUU TENA,

    ReplyDelete
  4. du!! sikujua kua wamesha mwonja

    ReplyDelete
  5. mambo ya Ngoswe tumwachie Ngoswe mwenyewe, me napita tu jamani...

    ReplyDelete
  6. mambo ya Ngoswe tumwachie Ngoswe mwenyewe, me napita tu jamani...

    ReplyDelete
  7. t sucks being a ceb...

    ReplyDelete

Top Post Ad