POLISI WAHAHA TUKIO LA KUMWAGIWA TINDIKALI BOSS WA HOME SHOPPING CENTER

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

WAKATI hali ya mmiliki wa maduka ya Home Shopping Centre, aliyemwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana, Said Mohammed Saad, ikiendelea kuimarika kutokana na matibabu anayopata, hakuna mtuhumiwa aliyekamatwa kutokana na tukio hilo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Kinondoni, Camilius Wambura, alisema polisi wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo.

“Jamani mambo mengine ni ya ndani ya polisi na si vema tukayatoa hadharani, tulieni jamani, upelelezi ukikamilika tutawaita na kutoa taarifa,” alisema Kamanda Wambura.

Saad alimwagiwa tindikali hivi karibuni maeneo ya Msasani City Mall, jijini Dar es Salaam na mtu asiyejulikana.

Baada ya tukio hilo, mtu huyo ambaye hadi sasa hajakamatwa, alikimbia na kutokomea kusikojulikana.

Taarifa za kipolisi zilieleza kwamba, Saad alimwagiwa tindikali akiwa anazungumza na mfanyakazi wa duka lake lililopo kwenye Jengo la Msasani City Mall.

Tukio la kumwagiwa tindikali mfanyabiashara huyo, limekuja ikiwa ni wiki mbili tangu Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Said Juma Makamba, ajeruhiwe vibaya usoni kwa kumwagiwa majimaji yanayosadikiwa kuwa ni tindikali.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Rais wetu kwa kuona wagonjwa na kwenda misibani 2 hajambo.

    ReplyDelete
  2. Ndio kipaji alichojaaliwa na mwenyezi Mungu. Unataka aende disko au ashinde baaa?

    ReplyDelete
  3. Ndio kipaji alichojaaliwa na mwenyezi Mungu. Unataka aende disko au ashinde baaa?

    ReplyDelete
  4. hahahaa watanzania kwa vichekesho na kudatana wallahi munanibamba! duh karibuni naona nikija kuishi huko!

    ReplyDelete
  5. Hahahahahahahahaha yeah ana kipaji mithili ya Messi kwa football.

    ReplyDelete

Top Post Ad