TANZANIA YAUMBULIWA....GAZETI MAARUFU LA MAREKANI LAANIKA UKATILI UNAOTENDEKA NCHINI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Tanzania imekosolewa  na  gazeti  maarufu  la  Marekani  wakati Rais Obama akipokewa kwa nderemo na  vifijo.
Gazeti hilo  maarufu nchini Marekani la The New York Times, limechapisha habari za kuonesha matukio ya ukatili yanayofanyika Tanzania.
 Habari hiyo iliyochapishwa katika toleo lake ya Juni 30, imeleza tukio la kuteswa na kuumiza kwa kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen Ulimboka.

Mwandishi wa habari hiyo amejaribu kunukuu kauli ya Dk. Ulimboka akieleza jinsi alivyotekwa na kuteswa kinyama kisha kutupwa kwenye Msitu wa Mabwepande.
Mwandishi  huyo  amesema kuwa Tanzania inaheshimika nje ya nchi kama kisiwa cha amani ndani ya ukanda wenye machafuko wa Afrika  Mashariki.
Kwamba kutokana na sifa hizo, Tanzania imejizolea sifa na ufadhili wa fedha kutoka kwa mataifa mbalimbali yaliyoendelea, ikiwamo Marekani, ambayo mwaka jana
iliipatia zaidi ya dola milioni 480.

Alisema kuwa wakati Rais Obama akiwasili Tanzania makundi ya kutetea haki za binadamu na chama kikuu cha upinzani wanasema matukio ya vitisho na ukandamizaji wa wapinzani wa kisiasa yanashika kasi. “Kuna woga, si amani”.
Ananukuu kuwa waandishi wamekuwa wakishambuliwa na
mmoja aliuawa akiwa anatekeleza kazi yake ya uandishi wa habari.

Aliongeza kuwa Julai mwaka jana, serikali ililifungia gazeti huru la uchunguzi la kila wiki la Mwanahalisi, ambalo lilikuwa likiandika kwa undani kuhusu tukio la kutekwa na kuteswa kwa Dk. Ulimboka, ambalo lilihusisha uhalifu huo na serikali ya Rais Kikwete.
Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari yenye makao makuu yake New York nchini Marekani, wiki jana ilimtaka Rais Obama kuliibua suala la uhuru wa vyombo vya habari atakapokutana na Rais Kikwete jijini Dar es Salaam.
Gazeti hilo pia limetaja vurugu za kisiasa kuwa zilichukua sura mpya na ambayo haikutegemewa wakati bomu la kurushwa kwa mkono lilipolipuliwa katika mkutano wa
hadhara wa kampeni za uchaguzi wa madiwani wa
CHADEMA na kusababisha vifo vya watu wanne mkoani Arusha.


Source:http://www.nytimes.com/2013/07/01/world/africa/violent-episodes-grow-in-tanzania-an-african-haven.html?_r=0
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. dah kweli vijana mmeongea sana.ila inaonekana hao wenye silaha na wenye kuichafua serikali mnawajua sasa si muwataje tu jamani.maana naona mnapindisha maneno hapo juu

    ReplyDelete
  2. Unafiki wa serikali ya ccm unafikia ukingoni.Kujaribu kuzuia nguvu ya ya umma ya mageuzi ni sawa na wendawazimu wa kuzuia mafuriko kwa mikono.Hongera New York Times!

    ReplyDelete
  3. Breaking News,Serikali ya ccm,kupitia kwa waziri wake wa habari George Mkuchika imelifungia gazeti la NewYork Times milele.Gazeti hilo linatuhumiwa kwa kuichana live serikali na kuandika jinsi mikono yake ilivyochafuka damu za raia wake iliyowaua. Mhariri .

    ReplyDelete
  4. Dun!New York Times na Mwanahalisi ni dugu moja.

    ReplyDelete

Top Post Ad