'IDD AZZAN HAUZI UNGA'

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

WAKATI Jeshi la Polisi Tanzania likiweka bayana kwamba, linamchunguza Mbunge wa Kinondoni kwa ‘leseni’ ya CCM, Mheshimiwa Idd Mohamed Azzan kama kweli anajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, baadhi ya wapiga kura wake wameibuka na kuthubutu kusema kiongozi huyo hauzi unga.
Wakizungumza na Uwazi juzi Bamaga, Mwenge jijini Dar, wapiga kura hao kutokea CCM, walisema madai kwamba mbunge wao ni mfanyabiashara wa ‘unga’ yamewashangaza sana.
Walisema haiingii akilini hata kidogo kwa mtu ambaye amepata utajiri wake huku majirani wakimuona halafu aangushiwe kashfa ya kufanya biashara hiyo haramu.
“Sisi hapa (Magomeni Makanya) tunamjua Idd tangu zamani akiwa kijana mdogo. Alikuwa na teksi akiwa anaendesha mwenyewe, akaja akanunua ya pili.
“Mwaka 1986 aliziuza, akanunua daladala aina ya Costa, akawa anaendesha mwenyewe, tena ilikuwa inafanya safari za Pugu Kariakoo, akaja akanunua lori, akawa anaendesha mwenyewe,” alisema mzee Mussa, mkazi wa eneo hilo.
Naye Bakari au maarufu kwa jina la Jabu, alisema yeye anakumbuka mwaka 1986, mheshimiwa akiwa anasaka maisha alifanya biashara ya kupeleka redio Bujumbura nchini Burundi kisha anarudi na mashati yalikuwa maarufu kwa jina la Juliana, anauza Dar, tayari kipindi hicho Idd  ana fedha zake.
“Sasa leo wanapozuka watu na kusema anauza dawa za kulevya, tunashangaa sana. Sisi majirani zake achilia mbali kuwa wapiga kura wake tungejua.
“Watu wanaojazana nyumbani kwake kabla hajaamua kuikarabati hii nyumba hapa wengi ni wale wenye matatizo, wanaomba msaada,” alisema mzee huyo.
Mzee mwingine, Hussein alisema anakumbuka mwaka 1989, yeye alikuwa shahidi wakati Azzan alipokopeshwa semi trela aina ya Mercedes Benz na kaka yake kwa makubaliano ya kumlipa fedha mwaka 1992.
“Azzan alikubali masharti hayo, akawa anaendesha mwenyewe kwenda nje ya nchi. Alikuwa akienda Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi mpaka Kongo.
“Na alikuwa akirudi anatubebea zawadi za chakula wazee wake kwa sababu ya ukaribu, mwaka elfu moja mia tisa na tisini na mbili alilipa deni, semi trela ikawa yake na akanunua jingine kama hilo.
“Nakumbuka kuna mwaka alipata ajali mbaya sana kule Ngara, akaumia na kulazwa, tukapata taarifa.
“Alipotoka akaamua kuanzisha Kampuni ya Azzan Investment na kununua mabasi mengi ya kukodisha, ndivyo ninavyojua mimi asili ya utajiri wa huyu bwana. Azzan hauzi unga bwana,” alisema mzee huyo.
Siku hiyohiyo, Uwazi lilimtafuta kwa simu Mheshimiwa Azzan na kumuuliza kama anawajua wazee hao ambapo alisema ni wazee wake anaowaheshimu sana, lakini akaomba asiongee kwa undani sana kwa vile alikuwa kikaoni.
Hivi karibuni, mtu mmoja aliyedai yupo jela Hong Kong, China kwa ishu ya unga aliandika majina ya watu aliodai ndiyo wafanyabiashara wa madawa ya kulevya na kuyatumbukiza majina hayo mtandaoni. Miongoni mwa majina hayo limo la Idd Azzan.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hiyo ni kweli kabisa toka nianze kumjua idd azan sijawahi kusikia wala kuona anauza madawa ya kulevya ,huyu anauza magar aina ya costal yaani mambo ya madawa ya kulevya hayamuhusu kabisa ,ni uchafuzi wa cv za watu ,mim niko magomeni kitambo na list ya wauza unga idd azan hayupo kabisa wamemsingizia ,,by dulla big migomigo

    ReplyDelete
  2. Akifikishwa mahakamani mtaenda kumtetea au vipembezoni mnaongea kwa uhuru.?.

    ReplyDelete
  3. Pumbavu sasa yeye ni the don ana watu wake wa chini ndo wanafanya iyo kazi hiv mbona mnakuwa hamna akili kwan hata majambaz wakubwa huwa hawaendi wao kuiba tumieni akili

    ReplyDelete
  4. We nawe kwani ndo mkewe mpka unasema ye ndo the don! Achaa

    ReplyDelete
  5. Hata mkewe anaweza asijue,wanaomtetea waende Polisi kusaidia uchunguzi

    ReplyDelete
  6. na wanao mtuhumu pia waende wakaisaidie polisi basi! acheni chuki zisizo na mpango, kwani kila mwenye hela mpaka auze unga?

    ReplyDelete
  7. Yote yanawezeka, cha msingi tuliachie jeshi la polisi lifanye kazi yake kwa haki kabisa na tutapata majibu.

    ReplyDelete
  8. Watu viherehere kweli

    ReplyDelete

Top Post Ad