NILICHOKIONA UWANJA WA TAIFA MECHI YA YANGA NA ASHANTI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Napenda kuwapongeza wachezaji,wanachama na mashabiki wa Yanga kwa ushindi wa kishindo wa goli 5 kwa 1.
1: Ukaguzi wa tiketi na rushwa.
Kuna wakati niliwahi kwenda kuangalia mechi kati ya Yanga na Simba,basi nikakata tiketi ya 15,000 lakini pale jukwaani nilipokaa,asilimia kubwa ya walionizunguka ni wale waliokuwa na tiketi za 3,000 na kinachofanyika wanatoa hongo ya sh 1,000 kwa maaskari then wanaruhusiwa kukaa jukwaa la 15,000.Hivyo hivyo na jana ndio utaratibu uliokuwa ukifanyika,waziwazi kabisa!Hivi hili TFF hili hamlifahamu?

2: Usafi wa viti na vyoo!
Nimekuwa nikijiuliza maswali bila kupata majibu,hivi zile hela zinazokatwa kila mechi kwa ajili ya uwanja zinafanya kazi gani?Nimekuwa nikihudhuria mechi pale taifa mara nyingi sana lakini kila siku mambo ni yale yale,viti vichafu,vyoo vichafu sana kupindukia.Jamani hela tunayotoa kama viingilio ni kubwa sana hizo huduma za usafi zifanyike,na kama kuna watu wanachukua hizo hela za usafi wakati usafi haufanyiki wawajibishwe.

Najua wahusika wamo humu,wayafanyie hayo kazi.Pia wale waliokuwa uwanjani jana na wale wenye uzoefu na uwanja wa taifa karibu tuchangie!


Source:Jamii forums
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad