PONDA ASIMULIA YA GEREZANI SEGEREA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KWA mara ya kwanza tangu apelekwe katika Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam wiki iliyopita, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, amezungumzia hali ilivyo katika gereza hilo. Akizungumza kupitia kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, Sheikh Ponda ameonyesha kuridhishwa na huduma anazopata katika gereza hilo.

Profesa Lipumba alimkariri Sheikh Ponda, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kumtembelea gerezani kiongozi huyo wa Kiislamu. “Nimekwenda pale Segerea na kufuata taratibu zote za kutaka kumuona Sheikh Ponda, nashukuru walinielewa na kunikutanisha naye katika chumba maalumu na kufanya naye mazungumzo.

“Kwa mujibu wa maelezo ya Sheikh Ponda, anapewa huduma zote na dawa zake zilizoachwa Hospitali ya Taifa Muhimbili zimepelekwa na anaendelea na matibabu vizuri, kidonda chake kinasafishwa vizuri na ana godoro lake la kulalia.

“Hata mimi nimeridhishwa na mazingira anayoishi gerezani, tuliweza kuelewana vizuri katika mazungumzo yetu.

“Amewasifia askari magereza kwa weledi wao wa kujali mtu tofauti na ilivyo kwa askari polisi ambao wamekuwa chanzo cha vurugu na uvunjifu wa amani ya nchi.

“Kwa taarifa ambazo nimeelezwa, ni kwamba Sheikh Ponda hajapasuliwa mishipa ya bega alilopigwa risasi na imekuwa ni bahati nzuri kwani imeonekana risasi ilipenya kwenye nyama.

“Si kwamba Sheikh Ponda anafurahia maisha ya gerezani, bali yuko huko kwa sababu ametakiwa kuwapo, kwa hiyo, CUF na Waislamu wote, tunaomba aachiwe,” alisema Profesa Lipumba.

Katika mazungumzo yake, aliwataka Watanzania kuungana pamoja katika kupinga vitendo vya ukatili vinavyofanywa na askari polisi nchini.

Alisema kwamba, chama chake kimechoshwa na ukatili unaofanywa na askari hao na kwamba ukatili huo uweze kukomeshwa, lazima Watanzania washirikiane kuupinga.

“Leo polisi ndiyo wanaoshirikiana na majambazi kufanya uhalifu, polisi hao ndiyo wanaoshirikiana na wauza unga na polisi hao hao, ndiyo wanaosahau wajibu wao wa kulinda raia na mali zao.

“Polisi hao wamekuwa wakijihusisha na mambo yasiyo na maadili na kulifanya Jeshi la Polisi lionekane la kihuni kwa sababu wananchi wanakosa imani nalo. Kwa hiyo, tunataka tume huru ya uchunguzi wa tukio la Sheikh Ponda na tunataka askari aliyehusika afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

“Jambo jingine la muhimu kwa wanasiasa wenzangu ni kwamba tuungane ili kuonyesha ushirikiano pale mmoja wetu anapopata matatizo na pia isiwe kwa wanasiasa peke yao bali pia kwa Mtanzania yeyote,” alisema.

Wakati huo huo, Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, zimemtaka Rais Jakaya Kikwete, kuunda tume huru kuchunguza tukio la kupigwa risasi Sheikh Ponda.

Mbali na tume hiyo, pia wanawataka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, wawajibike.

Katika mkutano wa dharura wa Waislamu uliofanyika jana katika Uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke Dar es Salaam jana uliokuwa na lengo la kujadili hatua za kuchukua kuhusu suala la hilo, walisema wanataka tume isiyokuwa na polisi kwa kuwa wao ni watuhumiwa.

Sheikh Kondo Juma wa taasisi hiyo, alisema Kamanda Shilogile ni mtuhumiwa wa kwanza kwani ndiye aliyetoa amri ya Sheikh Ponda kupigwa risasi.

“Tunatoa muda, kama hawakuwajibishwa, basi tutaandaa maandamano ya Waislamu wote nchi nzima, kwa kuwa tunaamini Ponda si mchochezi, kama angekuwa mchochezi nchi isingetawalika.

“Dalili za Ponda kupigwa risasi zilianza tangu tukiwa hapa Dar es Salaam wakati wa Iddi mosi kwani baada ya Baraza la Iddi katika Msikiti wa Mchangani, polisi walisema tukienda Morogoro watu wote waongee kasoro Ponda, sisi tukasema tutakwenda na tutaongea.

“Tukiwa Morogoro, gari yetu ilivamiwa na polisi ambao walikusudia shari na hawakuwa na lengo la kumkamata tu, lengo lilikuwa ni kumuua, tukaachana na Ponda kama mita 100 hivi, baada ya muda ndio nikapata taarifa kuwa amepigwa risasi,” alisema Sheikh Kondo.

Naye Sheikh Ameir kutoka Zanzibar, alisema kuna taarifa serikalini zinasema kuwa, tukio la kumwagiwa tindikali kwa raia wa Uingereza chanzo chake ni Ponda, ambapo alisema matukio ya kumwagiwa tindikali visiwani humo yako tangu miaka saba iliyopita.

“Alimwagiwa tindikali Sheikh Soraga, si mzungu yule, lakini pia gazeti la Telegraph la Uingereza limesema, matukio ya kumwagiwa tidikali nchini humo, yamekithiri, sasa tutaamini vipi kama si wazungu wamefanya tukio lile?.

“Kwa muda ambao wasichana wale wanadaiwa kumwagiwa tidikali, asilimia 99 ya Wanzanzibar walikuwa wanafuturu, hivyo watu wasithubutu kuunganisha tukio hili na Uislam.

“Hata hivyo, tunasikitika kwamba, Sheikh Ponda hakutendewa haki kuchukuliwa akiwa hospitali anaumwa, lakini siku zote haki haiombwi kwa hiari, ikishindikana tutajiandaa kuidai,” alisema.

Kwa upande wake, Sheikh Hussein Ismail, alisema kupigwa risasi kwa Sheikh Ponda ni kama wamepigwa Waislamu wote na akawataka kuchangia fedha za kuendesha kesi hiyo, fedha ambazo zilichangwa viwanjani hapo lakini hazikuhesabiwa.

Alisema watatumia utaratibu wa kufuata sheria na majukwaa hadi haki itakapotendeka kuhusiana na suala hilo.

Source:Mtanzania
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Serkal ya tanzania haina din,mnatwambiaje ponda sio mchochezi wakati amesema anataka uislam ushike dola??? Na wewe lipumba na cuf mclaan upande 1 mnatakiwa klaan na uchochezi wa ponda, eti aachiwe, aachiwe!!!!!!!??

    ReplyDelete
    Replies
    1. Prof. Lipumba usitake kuhalalisha kauli kwamba CUF ni chama cha Waislamu!!. Ni vizuri ukasema wewe kama wewe unataka Ponda aachiwe mara moja. Kukamatwa kwa Ponda kunatokana na makosa ya uchochezi wa kidini anaofanya. Kama si kweli kwanini wewe kama kiongozi usisubiri sheria ikachukua mkondo wake? Au unafikiri njia hiyo ya kumtetea Ponda na kutaka aachiwe bila hata sheria kuchukua mkondo wake kwa sababu ni muislamu ndo utaenda Ikulu kwa kura za waislamu? Mbona baadhi ya waislam haohao wanampinga Ponda. Katika mauaji na mapadri na wachungaji, uchomaji wa makanisa ulisema nini kama kiongozi? Kwa akili yako ya U-profesa unafikiri Ponda haenezi uchochezi wa machafuko ya kidini nchini? au kwa sababu ni uislam na wewe ni muislam hakuna shida?. Ni kweli Ponda anataka uislam uchukue Dola mimi naelewa maana yake ni kwamba nchi iendeshwe kiislam, kwa sababu hata aliyeshikilia dola kwa sasa ni muislam ila bado nchi haiendeshwi kiislam na ndo kasoro kwa Ponda. Sijawahi kufikiri kama kuna kiongozi anayeweza kuweka hadharani ubaguzi wake wa dini kama ulivyofanya. Napenda kukuhakikishia amani ya nchi hii itaendelea kulindwa kwa kuhakikisha kila mtu anaheshika na kudhaminiwa utu wake bila kujali rangi, kabila wala dini yake. Uchochozi wa watu kama Ponda na wewe (Sio CUF) utamulikwa popote ulipo, acheni kutamani damu za watu kama majini. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika, Mungu mbariki Sheik Ponda na Lipumba watambue kuwa ulimwengu na nchi hii ni ya watu wote na sii waislamu tu. Kila mwili umejengwa kwa nyama na mifupa na visu, mapanga, risasi na mabomu hayana dini atakayekutwa atakufa tu bila kujali dini yake.
      Reply

      Delete
  2. Prof. Lipumba usitake kuhalalisha kauli kwamba CUF ni chama cha Waislamu!!. Ni vizuri ukasema wewe kama wewe unataka Ponda aachiwe mara moja. Kukamatwa kwa Ponda kunatokana na makosa ya uchochezi wa kidini anaofanya. Kama si kweli kwanini wewe kama kiongozi usisubiri sheria ikachukua mkondo wake? Au unafikiri njia hiyo ya kumtetea Ponda na kutaka aachiwe bila hata sheria kuchukua mkondo wake kwa sababu ni muislamu ndo utaenda Ikulu kwa kura za waislamu? Mbona baadhi ya waislam haohao wanampinga Ponda. Katika mauaji na mapadri na wachungaji, uchomaji wa makanisa ulisema nini kama kiongozi? Kwa akili yako ya U-profesa unafikiri Ponda haenezi uchochezi wa machafuko ya kidini nchini? au kwa sababu ni uislam na wewe ni muislam hakuna shida?. Ni kweli Ponda anataka uislam uchukue Dola mimi naelewa maana yake ni kwamba nchi iendeshwe kiislam, kwa sababu hata aliyeshikilia dola kwa sasa ni muislam ila bado nchi haiendeshwi kiislam na ndo kasoro kwa Ponda. Sijawahi kufikiri kama kuna kiongozi anayeweza kuweka hadharani ubaguzi wake wa dini kama ulivyofanya. Napenda kukuhakikishia amani ya nchi hii itaendelea kulindwa kwa kuhakikisha kila mtu anaheshika na kudhaminiwa utu wake bila kujali rangi, kabila wala dini yake. Uchochozi wa watu kama Ponda na wewe (Sio CUF) utamulikwa popote ulipo, acheni kutamani damu za watu kama majini. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika, Mungu mbariki Sheik Ponda na Lipumba watambue kuwa ulimwengu na nchi hii ni ya watu wote na sii waislamu tu. Kila mwili umejengwa kwa nyama na mifupa na visu, mapanga, risasi na mabomu hayana dini atakayekutwa atakufa tu bila kujali dini yake.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Prof. Lipumba usitake kuhalalisha kauli kwamba CUF ni chama cha Waislamu!!. Ni vizuri ukasema wewe kama wewe unataka Ponda aachiwe mara moja. Kukamatwa kwa Ponda kunatokana na makosa ya uchochezi wa kidini anaofanya. Kama si kweli kwanini wewe kama kiongozi usisubiri sheria ikachukua mkondo wake? Au unafikiri njia hiyo ya kumtetea Ponda na kutaka aachiwe bila hata sheria kuchukua mkondo wake kwa sababu ni muislamu ndo utaenda Ikulu kwa kura za waislamu? Mbona baadhi ya waislam haohao wanampinga Ponda. Katika mauaji na mapadri na wachungaji, uchomaji wa makanisa ulisema nini kama kiongozi? Kwa akili yako ya U-profesa unafikiri Ponda haenezi uchochezi wa machafuko ya kidini nchini? au kwa sababu ni uislam na wewe ni muislam hakuna shida?. Ni kweli Ponda anataka uislam uchukue Dola mimi naelewa maana yake ni kwamba nchi iendeshwe kiislam, kwa sababu hata aliyeshikilia dola kwa sasa ni muislam ila bado nchi haiendeshwi kiislam na ndo kasoro kwa Ponda. Sijawahi kufikiri kama kuna kiongozi anayeweza kuweka hadharani ubaguzi wake wa dini kama ulivyofanya. Napenda kukuhakikishia amani ya nchi hii itaendelea kulindwa kwa kuhakikisha kila mtu anaheshika na kudhaminiwa utu wake bila kujali rangi, kabila wala dini yake. Uchochozi wa watu kama Ponda na wewe (Sio CUF) utamulikwa popote ulipo, acheni kutamani damu za watu kama majini. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika, Mungu mbariki Sheik Ponda na Lipumba watambue kuwa ulimwengu na nchi hii ni ya watu wote na sii waislamu tu. Kila mwili umejengwa kwa nyama na mifupa na visu, mapanga, risasi na mabomu hayana dini atakayekutwa atakufa tu bila kujali dini yake.
      Reply

      Delete
  3. Ivi wale wachungaji wanaoitanaga kwenye viwanja na kutoa mahubiri Yao kwa wakristo mbona hawapigwi risasi? leo mtu asihubiri mambo yanayohusu Dini yake eti anachonganisha.... Au kisa mwislam. Mtukome na m2ache. Laana Tu lwahi nyie

    ReplyDelete
  4. Kwani nani aliyemuua padro? Nan aliyelipua kanisa? Uislam unajitosheleza hauitaji demokracy so bora tugawane nchi kama sudan ili waislam tuongozwe na quran na sunna na MAKAFIRI waongozwe kikafiri vinginevyo Tanzania waislam=makafiri wote JAHANNAM, Nan yupo tayar kuingia jahannam?

    ReplyDelete
  5. serikali ya tanzania haina dini ukitaka uchochezi wako wa kidini kaombe uraia wa syria,pakstan,iran,saudi hapa kwetu ni kuwachapa risasi tu enzi za mwalimu hatukuwa na mambo ya kijingajinga kama haya

    ReplyDelete
  6. risasi ni spesheli ajili ya waislam makafiri yakiandamana yanatawanywa kwa mabomu ya machozi lipumba ameongea kama binadam na haki za kibinadam nyie makafiri mkiambiwa ukweli ndio inaitwa uchochezi waislam wa nchi hii wana nini wakati rais wenu kafiri alipotawala nchi hii kila kitu aliwapa bugando muhimbili kcmc kila kitu MSHAHARA KUANZIA MFAGIAJI MPAKA DAKTARI UNATOKA SERIKALINI MAPATO YA HOSPITALI YOTE YANAINGIA KANISANI waislam kimyaaaaaaaaaaaaaaa huo ni nini eti serikali haina dini serikali hii serikali hii ni ya kikafiri sie waislam hatuna chetu tumekaa kama wapangaji ndani ya nyumba


    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyo kafiri unayemuita bla yeye hata leo hii cdhan kama ungejua kuna kitu kinaitwa blog! Mtu kahangaika na kapgania uhuru ambao tunaufaidi had leo alaf bdo unamshtumu! Jarbu kufkiri kabla hujasema kitu! Jarbu kuangalia watu wanavyoteketea misri kama kuku wa manyanya! Je unataka na huku kuwe kama kule?

      Delete

Top Post Ad