SHILOLE ASHUSHIWA KIPIGO KISA MADENI...

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msanii nyota kwenye tasinia ya muziki na filamu bongo Zuwena Mohamed “ Shilole” mwishoni mwa wiki iliyopita alionja joto ya jiwe baada ya kutiwa mtu kati na wakina dada waliokuwa wanamdai kiasi kikubwa cha pesa.

Habari za uhakika zilizothibitishwa na mmoja wa wakina dada hao waliokuwa wanamdai zilisema kuwa wanawake hao waliamua kuchukua hatua za kumtia adabu Shilole baada ya kupata taarifa kuwa siku hiyo alikuwa ana hama kwa kukimbia na teni lao “ Ishu ilikuwa hivi sisi tunamdai huyu dada lakini cha kushangaza amekuwa akitupiga chenga sana na ona alivyokuwa sio mstaarabu kumbe siku hiyo alikuwa anahama na deni letu ndio maana tuliamua kwenda kumzingua” Alisema dada huyo aliomba jina lake lihifadhiwe.

Dada huyo aliendelea kufunguka mengi kuhusu sakata hilo “ Unajua sisi tunafanya biashara zetu hivyo kuna siku Shillole alikuja na kusema amekwama kipesa hivyo tumuazime pesa na tukafanya hivyo lakini cha kushangaza mwezi wa sita huu hataki kurudisha na amekuwa akitukwepa mara kwa mara hivyo majirani ndio wakatushtua kuwa anataka kuhama kwa staili ya kutoroka na deni letu ndipo tulipoenda wanawake wanne na kumshushia kipigo” Alisema dada huyo

Baada ya taarifa hizo Shilole alitafutwa kupita simu yake ya mkononi pamoja na kupita kwenye makoloni yake hakuweza kupatikani isipokuwa majirani mbalimbali walikili kutokea kwa tukio hilo la kufedhehesha kwa msanii huyo.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MREMBO KAMA WW KWELI UNAKUWA NA MADEN "HV N KWELI AU MTANDAO UNATANIA TU DU POLE ...LAKN MJN SHULE

    ReplyDelete
  2. dada umeshndwa kumpata mdhamin hapo dr na kwa urembo ulio nao du labda unaproblem pole

    ReplyDelete
  3. Sitaki kuamini...

    ReplyDelete
  4. baada ya kumpga mmepata ela zenu au??

    ReplyDelete
  5. Huo ni uwongo mnmeshaanza kuchafua watu mbwa nyinyi.

    ReplyDelete
  6. Inakuaje STAR halafu unashindwa kulipa deni bongo bado hatujui nini maana ya STAR. star sio kuonekana kwenye TV first ur bank Account inacheka sio kila siku mchangiwe madeni mnatia aibu

    ReplyDelete
  7. kama ni kweli ni aibu sana. huyu ndo anatarajiwa kufanya collabo na JLo? dah...kazi tunayo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Vichekesho kweli..Hakuna colabo na Jlo wala nini ni wajanja wa mjini wametia usanii ili wafanye mambo yao na sasa wamemaliza kula vyao imebakia colabo tuuu..

      Delete
  8. hapana huu ni uongo na utakuwa umesambazwa hili kumchafulia tu dada kazana kwenye game unaua sana achana na hao wambea vishakunaku

    ReplyDelete
  9. Hilo ndo tatizo wasanii wengi wa bongo wanaishi maisha feki..so sishangai mambo kama hayo kutokea..

    ReplyDelete
  10. Nyie DC WASHINGTON,mnamsaidiaje sasa,sio kumrusha kiuchafu chafu tu.Alipokuwa huko kila kona mnaye mpaka kashindwa DO,Kaja nazo huko na karudi nazo huku.

    ReplyDelete
  11. sio kli mbona hmajaeka picha sas zikimuonesha kama kala kichapo , wcheni kuchafuwa watu , pumbavu zenuuuuu ,

    ReplyDelete

Top Post Ad