DINI YA AJABU YAANZISHWA MBEYA INAABUDU MUNGU ILA UCHAWI, POMBE NA UZINZI RUKSA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Habari Wadau:

Dini inayoamini katika MUNGU lakini ikiruhusu yale ambayo dini zingine zinapinga imeanzishwa eneo la mji mdogo wa Makongolosi wilayani Chunya mkoani Mbeya,

Dini hiyo haiamini katika kutoa sadaka bali inasema tunamtolea nani sadaka wakati Vitu vyote tulivyonavyo ni mali ya MUNGU,kwa nini tunampa MUNGU mali zake Mwnyewe.!

Dini hiyo inaruhusu ulevi,uchawi na uzinzi kwa sababu vimeumbwa na MUNGU,Vile vile inaamini hakuna dhambi duniani,Dini hiyo inaitwa DIMAYO, sasa imeanza kuenezwa Mbeya

=========================
Ufafanuzi
=========================

Quote By GAMBISHI DWESE View Post
Yawezekana kweli Bwana Domy umekutana nami. Mimi Ndiyo PAPA-DIMAYO 1: GAMBISHI DWESE,( nabii wa kwanza wa DIMAYO) hata hivyo pengine umeninukuu kimakosa.Kwanza kabisa Dimayo haiamini katika uwepo wa mungu muumbaji aliye hai wala aliyekufa anayedaiwa kuhusika na kila kinachoendelea ulimwenguni.

Na nimeshatoa kitabu kinachoitwa HAKIKA HAKUNA MUNGU MUUMBAJI ALIYE HAI WALA ALIYEKUFA anayehusika na kila kinachoendelea. kijitabu hiki kinaeleza kinagaubaga kwanini Dimayo haiamini katika uwepo wa mungu muuumbaji. nikipata nafasi nitakiingiza kwenye mtandao ili watu wengi wakisome.

Ni kweli hakuna kitu Dhambi bali kuna makosa. na kosa linaweza kuwa kosa kulingana na mazingira na wakati katika jamii tofauti. Na ni kweli kwamba dini yetu ni ya starehe wala si ya mateso, maana tunaamini hakuna maisha zaidi ya haya tuliyonayo. Dimayo haijampa mtu ruksa ya kuvunja kanuni halisi asili wala sheria halali ya serikali yake halali na wala haina upotoshaji hata kidogo. 

Kinachoitwa sadaka kwetu huwapa watu wenye matatizo. Ni kweli kuna michango mingine lakini ni ya hiari na ni kwa ajili ya ushirika. Ni kweli kwenye JUMADI (jumba la makutano la Dimayo kutakuwa na kaunta ya vinywaji). unajua kunywa na ulevi ni vitu viwili tofauti; ulevi ni tabia ya mtu ya kutumia vileo kupindukia, lakini kwetu tunasema kunywa uwezavyo ilimradi huumii wala kuumiza vyote kisaikolojia na kimwili, kwa mantiki hiyo ulevi kwetu noma ila unywaji ni safi.


Uchawi ni sayansi, ila utumike kwa faida siyo kwa kuleta madhara. kuwaambia watu eti acheni ngono eti mungu hapendi wataacha?. wambie wafanyeje ngono kulingana na wakati na mazingira. Dimayo inamfundisha mtu kutenda inavyofaa yanayofaa kutendwa kwa kufuata kha na kahaka. Anyway nashukuru kwa kuianzisha mada hii, nafikiri nitachukua nafasi kuielezea zaidi kila inavyowezekana. Nina uhakika kwa mtu yeyote mwenye uwezo mkubwa wa kutumia akili zake hawezi kupingana hata kidogo na DIMAYO.
JF
Udaku Specially Blog
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kweli dunia imevaa bukta yaani ushetaniwote ili dhehebu limebeba isije kuwa freemason wameanzisha kwa jina hilo na kanisa linaendeshwaje hao masonic2

    ReplyDelete
  2. Si bora hawa kuliko wanaouwa wenzao wasiokuwa na hatia

    ReplyDelete
  3. kwa mbeya sishangai kuna makanisa ya kila aina!!!!

    ReplyDelete
  4. furahini raha ya muda mfupi duniani huku mkidaganywa na baba wa uongo Lucifer.Ila the end is near ndipo mtajua kama kuna Mungu au Hakuna Mungu.Asomaye na afahamu.

    ReplyDelete
  5. UPOTOFU ULIODHAHIRI NA MUNGU HUMPELEKA MTU AKUTAKAYE mfano hata ukisema naabudu na kuiomba meli katika mambo yangu yote eti kwa kuwa yenyewe ni kubwa lakini inaelea kwenye maji (ignore law of floatation) na shilingi (sarafu) ni ndogo lakini inazama, mungu atakukidhia hayo uyahitajiayo ila tambua siku ya mwisho utakutana adhabu kali iumizayo kwa kuikataa haki na kuifuata batili na ndio maana tumegewa akili na hii ndio tofauti yetu na wanyama.
    USISAHAU KUSUDIO LA KUUMBWA KWAKO, MAISHA YA DUNIA NI MAFUPI NA YENYE KUDANGANYA NA ADHABU ZA MUNGU NI ZENYE KUUMIZA HASWAA.
    "kwa neema za mungu alizokupa tena bure mlipe kwa mema na sio kumkufuru, kila nafsi itaonja kifo"
    by MTUKUTU B4.

    ReplyDelete
  6. Teeeeeh......! Haya majanga sasa....! Kwel km hivo dunia #kushnei .....!

    ReplyDelete
  7. pia kuna dini hapa mbeya inaamini mungu wetu wanamsingizia tu hawez kuwachoma wenye dhambi bal atawaokoa siku ya mwisho brother wangu ni paster kwenye hlo chuch 2nakoelekea sijui

    ReplyDelete
  8. Nina watu wengi nawajuwa hawaani kama Mungu anaitwa Mungu na hawaamini kama yuko mbinguni na wala hawaamini prayers(maombi)! Wenyewe wanaamini kuna kitu kipo kinatuangalia nawala hakipo mbinguni bali hewani kinatuzunguka!! Pia wanaamini kutenda wema nakumsaidia wasio jiweza, huwa hawaombi duwa kabisa..maombi kwao ni no. Ila wanaroho nzuri sana tena sana kushinda hata sisi tunao muabudu Mungu! Kusema kwao dini ni imani na hakuna mwenye kujua ukweli coz vitabu vimeandikwa na watu kama sisi(stories) so kama huna imani nivigumu kuamini mambo ya dini na kama hujakulia mazingira ya dini ndio kabisaaa.

    ReplyDelete

Top Post Ad